• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 5:50 AM
Ulinzi Starlets yamsajili straika matata Joy KingLady Oriyo

Ulinzi Starlets yamsajili straika matata Joy KingLady Oriyo

NA RUTH AREGE 

KLABU ya Ulinzi Starlets ya Ligi Kuu ya Wanawake nchini (WPL), imemsajili straika matata Joy KingLady Oriyo kutoka Zetech Sparks.

Tayari kocha wa Zetech Bernard Kitolo amethibitisha kuwa mshambulizi Oriyo ameigura timu hiyo na kujiunga na wanajeshi.

“KingLady Oriyo amejiunga na Ulinzi Starlets, tulimshauri asalie na sisi msimu ujao lakini tayari Ulinzi walikuwa na ofa nzuri. Walikuwa wameahidi kazi ya Jeshi la Ulinzi (KDF),” alisema Kitolo.

Kitolo alisema klabu hiyo ‘ilifanya kila kitu’ kujaribu kumshikilia lakini straika huyo alichagua kutosalia na kumaliza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Zetech ili kujiunga na wapinzani wao.

Ahadi ya Ulinzi ya kumsaidia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kupata kazi ya KDF inaweza kuwa ilifanya vya kutosha kumwondoa mchezaji huyo kutoka Zetech.

Nae kocha wa Ulinzi Joseph Mwanzia anasema, kumsajili Oriyo ilikuwa njia mojawapo ya kuwa na ushambuliaji dhabiti msimu ujao.

“Wakati huu wa dirisha la uhamisho tumesajili tu mchezaji mmoja ambaye ni Oriyo. Atatusaidia pakubwa msimu kesho kwa mashambulizi,” aliongezea

Oriyo, alijiunga na Zetech mwaka 2021 baada ya kumaliza masomo yake ya Shule ya Upili akiwa na shule ya upili ya wasichana ya Kwale.

Alitegemewa na klabu ya Zetech msimu jana, aliisadia klabu hiyo kumaliza katika nafasi ya tano ligi ya WPL msimu jana.

Oriyo pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 20.

Disemba 2021, alipokea tuzo ya mchezaji bora wa mwezi na Chama cha Ustawi wa Wanasoka wa Kenya (KEFWA).

  • Tags

You can share this post!

Arsenal wakomoa Spurs ugani Emirates na kufungua pengo la...

Ruto atumia ‘BBI’ aliyoikataa kutunuku wandani

T L