• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Wakenya 4 waona giza tenisi ya Afrika ya Under-18 ikianza Tunisia

Wakenya 4 waona giza tenisi ya Afrika ya Under-18 ikianza Tunisia

Na GEOFFREY ANENE

WANATENISI wa Kenya wamefanya vibaya katika siku ya kwanza ya mashindano ya Bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 mjini Sousse, Tunisia mnamo Novemba 22.

Roselida Asumwa (nambari 1,400 duniani kwenye viwango bora vya chipukizi), Cynthia Wanjala (1,934) na Alicia Owegi (1,068) walipigwa katika kitengo cha kinadada cha mchezaji mmoja kila upande naye Derick Ominde hakuwa na lake kwa upande wa wavulana.

Asumwa alikuwa wa kwanza kufundishwa jinsi ya kucheza tenisi. Alilemewa na Amira Bargaoui (1,013) kutoka Tunisia kwa seti mbili kavu za 6-1, 6-1. Wanjala alipoteza dhidi ya Mzimbabwe Tanyaradzwa Midzi (627) 6-4, 6-1, naye Owegi akabanduliwa na raia wa Botswana Naledi Raguin (2,007) 5-7, 7-5, 7-5.

Ominde (765) amepepetwa na Mehdi Benchakroun (90) kutoka Morocco anayeorodheshwa wa kwanza katika kitengo hicho kwa 6-2, 6-0. Kael Shalin Shah (766) aliratibiwa kumenyana na Mmoroko Hamza El Amine (349) baadaye Jumatatu.

Owegi na Wanjala pia walifaa kushirikiana katika mechi ya wachezaji wawili kwa wawili baadaye Jumatatu, sawa na Asumwa na Angela Okutoyi. Okutoyi (pichani), ambaye anaorodheshwa 142 duniani, alipata tiketi ya bwerere katika raundi ya kwanza kwa hivyo ataanza kampeni yake ya mchezaji mmoja kwa mmoja katika raundi ya 16-bora dhidi ya mshindi kati ya Meriem Ezzedine (1,277) kutoka Tunisia na Rehab Mebarki (1,309) kutoka Algeria.

You can share this post!

Michael Carrick kushikilia mikoba ya Man-United hadi kocha...

Kipusa Mbuche kusajiliwa na TSC Queens ya Tanzania

T L