• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 8:55 AM
Wakenya sita kuwania ubingwa wa Pearl Rally Uganda

Wakenya sita kuwania ubingwa wa Pearl Rally Uganda

Na GEOFFREY ANENE

MADEREVA sita kutoka Kenya wako katika orodha ya 49 watakaoshiriki duru ya Mbio za Magari za Afrika (ARC) ya Pearl Rally nchini Uganda.

Karan Patel, ambaye anaongoza Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC), chipukizi wanaokuzwa na Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (FIA) McRae Kimathi, Jeremy Wahome, Hamza Anwar na Maxine Wahome pamoja na Nikhili Sachania watapeperusha bendera ya Kenya kwenye duru huyo ya tatu.

Akishirikiana na Tauseef Khan katika gari la Ford Fiesta, Patel alishinda duru ya pili ya ARC Equator Rally iliyofanyika katika maeneo ya Naivasha katika kaunti ya Nakuru mwezi uliopita.

Kimathi na mwelekezi wake Kioni Mwangi wamekuwa barani Ulaya kwa duru ya Mbio za Magari za Dunia (WRC) ya Croatia. Watapaisha gari la Subaru N10 badala lao la kawaida la Ford Fiesta R3.

Jeremy, ambaye alifanya vyema Equator Rally mwezi Machi baada ya kuwa nje miezi sita*, atashirikiana na Vicror Okundi katika Ford Fiesta R3. Maxine, ambaye alinyakua taji la mbio za magar za kinadada pekee la Lioness Rally katika kituo cha michezo cha Kasarani, atashirikiana na Waigwa Murage katika Subaru N10. Anwar na mwelekezi wake Adnan Din watashirikiana katika Mitsubishi Lancer EVO10. Sachania atashirikiana na Deep Patel katika Mitsubishi Lancer EVO10.

Bingwa wa duru ya kwanza ya Afrika, ambayo ilifanyika nchini Ivory Coast, Mzambia Leroy Gomes akishirikiana na mke wake Urshlla Gomes, watapaisha Ford Fiesta R5.

Madereva kutoka Rwanda, Burundi na Uganda pia watashiriki. Uganda ina idadi kubwa ya washiriki (39).

You can share this post!

Kikao cha Kibaki chageuzwa uwanja wa Azimio na Kenya Kwanza...

Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa walia bei ya juu ya...

T L