• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Zidane, Conte kati ya wakufunzi wa haiba wanaohusishwa na Newcastle United

Zidane, Conte kati ya wakufunzi wa haiba wanaohusishwa na Newcastle United

Na MASHIRIKA

NI rasmi kwamba Newcastle United kwa sasa wanatafuta kocha mpya baada ya kikosi hicho kuagana na mkufunzi Steve Bruce.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 60 anaagana na Newcastle siku 13 baada ya umiliki wa kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kutwaliwa na mabwanyenye wa Saudi Arabia waliokikununua kwa Sh47.6 bilioni.

Mechi ya mwisho kwa Bruce kusimamia kambini mwa Newcastle ni ile iliyowashuhudia wakipepetwa 3-2 na Tottenham Hotspur uwanjani St James’ Park. Mechi hiyo iliyokuwa yake ya 1,000 kusimamia katika taaluma ya ukufunzi ndio ya pekee aliyoiongoza chini ya wamiliki wapya wa Newcastle almaarufu ‘The Magpies’.

Kwa mujibu wa Bruce, kumekuwa na panda-shuka tele kambini mwa Newcastle tangu umiliki wa kikosi hicho ubadilike. Graeme Jones aliyekuwa msaidizi wa Bruce kwa sasa atakuwa mshikilizi wa mikoba ya Newcastle.

Newcastle wamefichua kwamba kocha mpya atakayemrithi Bruce atatangazwa hivi karibuni na nafasi hiyo inahusishwa na wakufunzi wengi

Kufikia sasa, Newcastle hawajashinda mechi yoyote katika kampeni za EPL msimu huu na wanashikilia nafasi ya 19 jedwalini baada ya kusajili sare tatu kutokana na mechi nane za ufunguzi. Newcastle watakuwa wageni wa Crystal Palace katika mchuano wao ujao ligini mnamo Jumamosi ya Oktoba 23, 2021 ugani Selhurst Park.

Bruce aliteuliwa kuwa kocha wa Newcastle mnamo Julai 2019 na akaongoza kikosi hicho kukamilisha kampeni za EPL katika nafasi za 13 na 12 mtawalia chini ya kipindi cha misimu miwili iliyopita.

Rafael Benitez, Antonio Conte, Lucien Favre, Paulo Fonseca na Steven Gerrard. Wengine ni Eddie Howe, Frank Lampard, Roberto Mancini, Roberto Martinez na kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Furaha kuu kafyu ikiondolewa

Mashujaa Dei: Ruto ‘apuliza vuvuzela’ Wakenya...

T L