• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 5:36 PM
Wan-Bissaka atozwa faini na kupigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miezi sita

Wan-Bissaka atozwa faini na kupigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miezi sita

Na MASHIRIKA

BEKI Aaron Wan-Bissaka wa Manchester United amepigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miezi sita na kutozwa faini ya Sh4.9 milioni.

Hii ni baada ya kukiri kwamba alivunja hatia za trafiki kwa kuendesha gari kabla ya kuhitimu kufanya hivyo na bila bima aliposimamishwa na polisi jijini Manchester mnamo Juni 23, 2021. Nyota huyo aliwahi pia kupatikana na hatia ya kuendesha gari kwa kasi mjini Bradford mnamo Septemba 2020 na alipotiwa nguvuni, hakuweza kuwasilisha stakabadhi muhimu alizoagizwa kutoa.

Baada ya kukosa kujibu barua muhimu zilizotaka ajieleze kortini, Wan-Bissaka alikuwa na kila sababu za kuadhibiwa. Wan-Bissaka, 24, sasa anaishi jijini Greater Manchester kwa pamoja na mchumba wake na mtoto wao wa umri wa miezi 12.

Gari lake aina ya Lamborghini Urus liliwahi kuhusika katika ajali ya barabani mnamo Aprili 2020 na Juni 23, 2021. Alitozwa faini ya Sh4.7 milioni kwa kosa la kuendesha gari kabla ya kuhitimu na Sh234,000 nyinginezo kwa kukosa kujieleza kuhusu kiini cha kuendesha gari kwa kasi.

Pia alitozwa kima cha Sh29,640 kulipia gharama ndogo ya kukarabatiwa kwa gari alilokwaruzana nalo huku akilipia Sh24,960 ambazo ni gharama ya kufikishwa kwake mahakamani.

You can share this post!

Pigo Arsenal baada ya majeraha na corona kuweka nje mabeki...

COVID-19: Mechi za EFL za Disemba 26, 2021 zaahirishwa

T L