• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Wanamichezo bora Kenya mwaka 2021 kutuzwa katika kaunti ya Kakamega Januari 2022

Wanamichezo bora Kenya mwaka 2021 kutuzwa katika kaunti ya Kakamega Januari 2022

Na GEOFFREY ANENE

SHEREHE za kutuza wanamichezo bora wa Kenya maarufu SOYA zitafanyika katika kaunti ya Kakamega mwezi Januari 2022.

Hii ni baada ya mwanzilishi wa tuzo hiyo Paul Tergat, ambaye ni rais wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) kusaini maelewano na Gavana wa Kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya mnamo Oktoba 7.

Rais wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) Paul Tergat akihutubu jijini Nairobi kwenye hafla ya awali. Picha/ Maktaba

Kakamega itakuwa kaunti ya nne kuandaa hafla hizo baada ya Nairobi, Mombasa na Nakuru.

Kauli mbiu ya hafla ya 2021 ni “Kutoka hali ya kujirekebisha hadi kupata nafuu tena.”

Washindi wa tuzo hiyo tangu ianzishwe mwaka 2005 ni Catherine Ndereba na Benjamin Limo (2005), Janeth Jepkosgei na Alex Kipchirchir (2006), muogeleaji Jason Dunford na Janeth Jepkosgei (2007), Samuel Wanjiru na Pamela Jelimo (2008) na mwanaraga Collins Injera na Linet Kirui (2009). Pia, kuna David Rudisha na Nancy Lagat (2010), Mary Keitany na David Rudisha (2012), Caleb Ndiku na Eunice Sum (2014) na mrushaji mkuki Julius Yego na Hyvin Kiyeng (2015), miongoni mwa wengine.

Washindi wa hivi punde wa tuzo hiyo ya kifahari ni nahodha mpya wa Harambee Stars Michael Olunga na mshindi mpya wa marathon kwenye Olimpiki Peres Jepchirchir. Walishinda makala ya 2020 yaliyofanyika mjini Naivasha katika kaunti ya Nakuru.

You can share this post!

MKF yawataka wanasiasa kuheshimu Rais Kenyatta wanaposaka...

Ni idadi ndogo tu ya wanaojitokeza Thika kujisajili wawe...