• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Wanaraga chipukizi wa Madagascar kuwasili Jumatano kwa kivumbi cha Barthes Trophy

Wanaraga chipukizi wa Madagascar kuwasili Jumatano kwa kivumbi cha Barthes Trophy

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande wasiozidi umri wa miaka 20 ya Madagascar itawasili Juni 30 kwa Kombe la Afrika (U20 Barthes Trophy).

Wanavisiwa hao watalimana na Senegal mnamo Julai 3 katika uga wa kitaifa wa Nyayo kabla ya kuchapana na wenyeji na mabingwa watetezi Kenya mnamo Julai 11.

Dimba hilo liling’oa nanga Juni 26 uwanjani humo ambapo vijana wa kocha Curtis Olago waliibuka na ushindi wa alama 50-3 baada ya kuongoza pembamba 13-0 wakati wa mapumziko.

Timu ya Kenya ya wachezaji 15 kila upande wasiozidi umri wa miaka 20 maarufu kama Chipu, ilikutana na Madagascar mara ya mwisho mnamo Machi 2018. Ilishinda mchuano huo kwa kukung’uta wanavisiwa hao 51-13 mjini Windhoek, Namibia.

Mshindi wa dimba hili hufuzu kushiriki mashindano ya dunia ya daraja ya pili (JWRT) ambayo Kenya iliwahi kuandaa 2009 na pia itakuwa mwenyeji wa makala ya 2022. Namibia, ambayo ilipoteza 21-18 katika fainali ya Barthes Trophy mwaka 2019 mjini Nairobi, haishiriki mashindano haya ya Afrika mwaka huu. Ilijiondoa baada ya kikosi chake kupatikana na virusi vya corona.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume ajitia kitanzi nje ya afisi ya ardhi Thika

Tuju adai ‘Tangatanga’ wamechoka