• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
White Cap yadhamini mbio za magari za akina dada pekee Lioness Rally

White Cap yadhamini mbio za magari za akina dada pekee Lioness Rally

Na GEOFFREY ANENE

KAMPUNI ya bia ya Kenya Breweries (KBL) kupitia kwa bidhaa yake ya White Cap Lager, itakuwa mshirika wa makala ya kwanza ya Mbio za Magari za Lioness Rally mwaka 2022.

Mbio hizo za kipekee zitahusisha kinadada pekee. Zitafanyika katika mashamba ya uwanja wa kimataifa ya Kasarani mnamo Machi 27.

Baadhi ya majina tajika yaliyothibitisha kuwania taji ni Lisa Christofferson na mtangazaji Pauline Sheghu. Christofferson ni mwanzilishi wa klabu ya Lioness Rally.

Si mara ya kwanza KBL imejitosa katika mbio za magari nchini mwaka huu kupitia White Cap.

Majuma machache yaliyopita, White Cap ilitangazwa kuwa mshirika wa kuburudika vileo kwa ustaarabu wa Mbio za Magari za Kitaifa Kenya (KNRC) na pia East African Classic Safari Rally.

Akizungumza jijini Nairobi wakati wa kutangazwa kwa udhamini na kuzinduliwa kwa Lioness Rally leo Jumatano, Christoffersen amefurahia kujihusisha kwa KBL katika mashindano hayo kwa kiwango kikubwa ikiwemo kuwa na waelekezi wa barabarani, madereva, makanika na waelekezi wa madereva.

Christoffersen alisema, “Tunafurahia usaidizi unaofanikisha mbio hizi na shughuli nyingine tunazopanga kufanya, hadi zitimizike.”

Sheghu aliongeza kuwa kinadada wanaweza kutimiza mengi kupitia ushirikiano.

Meneja wa Mauzo wa White Cap, Catherine Ndung’u alisisitiza umuhimu wa mbio hizo za magari za wanawake kuungwa mkono na pia ajenda ya kuhamasisha kuhusu jinsia katika mbio za magari. KBL inaadhimisha miaka 100.

 

  • Tags

You can share this post!

Uwanja wa Wembley kuwa mwenyeji wa gozi la Finalissima kati...

Ashtakiwa kumsababishia kero jirani akimshuku kanasa mume...

T L