• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Wolves wahakikishia mashabiki Lopetegui ataendelea kuwa kocha wa kikosi hicho msimu ujao wa 2023-24

Wolves wahakikishia mashabiki Lopetegui ataendelea kuwa kocha wa kikosi hicho msimu ujao wa 2023-24

Na MASHIRIKA

WOLVERHAMPTON Wanderers wamefutilia mbali tetesi kwamba wataagana na Julen Lopetegui na kusisitiza kuwa mkufunzi huyo raia wa Uhispania atasalia kuwa kocha wao msimu ujao wa 2023-24.

Lopetegui alianza kudhibiti mikoba ya Wolves mnamo Novemba 2022 kikosi hicho kikivuta mkia wa jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Licha ya kuwaongoza kusalia ligini muhula ujao, kumekuwa na uvumi kwamba mustakabali wake ugani Molineux ulikuwa ukining’inia padogo.

Mnamo Alhamisi, mkurugenzi wa soka kambini mwa Wolves, Matt Hobbs, alisema Lopetegui anafurahia maisha yake kambini mwa Wolves na ametoa hakikisho la kusalia nao hadi atakapofikia malengo ya kikosi.

Lopetegui, 56, amewahi pia kuwanoa masogora wa Real Madrid na timu ya taifa ya Uhispania na amewataka waajiri wake wa sasa kujitolea kadri ya uwezo wao na kumsaidia kusajili wanasoka wa haiba kubwa kwa ajili ya kampeni za msimu ujao wa 2023-24.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

  • Tags

You can share this post!

Mjukuu wa mzee wa kijiji aliyetuhumiwa kuiba maharagwe...

Msituombe damu ili mkaiuze, wakazi Murang’a wamwambia...

T L