• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Msituombe damu ili mkaiuze, wakazi Murang’a wamwambia Waziri wa Afya

Msituombe damu ili mkaiuze, wakazi Murang’a wamwambia Waziri wa Afya

Na MWANGI MUIRURI

WAKAZI wa Murang’a wameitaka serikali kuhakikisha inawajibika katika matumizi ya damu wanayotoa kwa hiari, wakiionya dhidi ya kugeuza ukarimu wao kuwa biashara.

Wakiongea mjini Murang’a katika hafla kuadhimisha siku ya utoaji damu nchini 2023, wenyeji hao walitoa onyo kwa serikali wakisema hawatataka kuona damu wanayojitolea kutoa inaingizwa ufisadi kupitia kuuzwa kwa wagonjwa hospitalini.

“Tukitoa damu kwa hiari na bila malipo, nayo isiende kuuziwa wagonjwa. Wapewe bure, bila kutozwa ada yoyote” akasema mkazi, Bw James Irungu.

Hafla hiyo iliyoandaliwa katika uwanja wa Ihura, ilihudhuriwa na Waziri wa Afya Bi Susan Nakhumicha pamoja na Balozi wa Hungary nchini Bw Zsolt Mèszaros.

Waziri wa Afya Bi Wafula Nakhumicha akihutubia wakazi wa Murang’a Juni 14, 2023 katika maadhimisho ya sikuu ya utoaji damu ulimwenguni katika uwanja wa Ihura. Picha|MWANGI MUIRURI

“Mimi nilishuhudia ndugu yangu akizuiliwa hospitalini kwa kukosa pesa za bili. Kati ya bili hiyo ilikuwa ni Sh36,000 za kuwekwa damu ilihali yeye alikuwa akijituma kutolewa damu kila mwito huo ukitangazwa,” akasema Bi Eunice Njagi.

Waziri Nakhumicha alitangaza kuwa serikali imeweka mikakati dhabiti kufuatilia damu yote iliyochangwa, lakini hakugusia suala nyeti la mauzo ya hospitalini kwa wagonjwa.

“Tunaweza tukajua damu yote iliyo katika hazina yetu iko wapi hadi itumike kwa mgonjwa,” akasema.

Alisema kwamba Wakenya ni wakarimu na huwa wanajitolea kwa utu ili kuhakikisha taifa liko na hazina ya damu.

“Ninafahamu Mkenya ambaye hadi sasa amechanga damu mara 102.”

Bi Nakhumicha alitangaza kufunguliwa kwa hazina ya damu katika hospitali kuu ya Murang’a na ambayo itakuwa ikihudumia wagonjwa wa eneo hilo na viunga vyake.

“Serikali itaweka mitambo ya Sh10 millioni katika kituo hicho na kitakuwa na uwezo wa kuweka damu kwa muda mrefu,” akasema.

Balozi wa Hungary nchini Kenya Bw Zsolt Mèszaros akihutibia wakazi wa Murang’a Juni 14, 2023 katika maadhimisho ya sikukuu ya utoaji damu ulimwenguni katika uwanja wa Ihura. Picha|MWANGI MUIRURI

 

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Wolves wahakikishia mashabiki Lopetegui ataendelea kuwa...

Uhispania waangusha Italia na kujikatia tiketi ya kuvaana...

T L