• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:15 PM
Wolves wamsajili kipa Jose Sa kuwa kizibo cha Rui Patricio aliyeyoyomea AS Roma

Wolves wamsajili kipa Jose Sa kuwa kizibo cha Rui Patricio aliyeyoyomea AS Roma

Na MASHIRIKA

WOLVES wamemsajili kipa raia wa Ureno, Jose Sa kutoka klabu ya Olympiakos kwa mkataba wa miaka mitano.

Kusajiliwa kwa Sa mwenye umri wa miaka 28 kunachochewa na hatua ya mlinda-lango matata Rui Patricio kuhamia AS Roma wanaotiwa makali na kocha Jose Mourinho.

Sa aliwajibishwa na Olympiakos mara 124 katika kipindi cha misimu mitatu ambapo alihudumu kambini mwa kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Uturuki. Alisaidia waajiri wake hao kutia kapuni mataji mawili ya Ligi Kuu.

Aliwahi kuhudumu kambini mwa Benfica chini ya kocha mpya wa Wolves, Bruno Lage aliyeaminiwa fursa ya kuwa kizibo cha Nuno Espirito aliyehamia Tottenham Hotspur.

Ingawa hajawahi kuwajibishwa katika kikosi cha watu wazima katika timu ya taifa ya Ureno, Sa alikuwa sehemu ya wachezaji waliounga kikosi cha akiba kwenye fainali ya Uefa Nations League 2019 iliyoshuhudia Ureno wakiwazamisha Uholanzi.

Sa alitegemewa pakubwa na Olympiakos kwenye mchuano wa mkondo wa kwanza wa Europa League uliowakutanisha na Wolves katika hatua ya 16-bora mnamo 2020-21.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Fainali ya UEFA 2023 sasa kuandaliwa Istanbul kutokana na...

West Brom wakataa ofa ya West Ham kwa ajili ya kipa wao...