• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:02 PM
Yatani apendekeza bajeti ya michezo kuongezwa hadi Sh15.8 bilioni

Yatani apendekeza bajeti ya michezo kuongezwa hadi Sh15.8 bilioni

NA AYUMBA AYODI

WAZIRI wa Fedha na Mipango ya Kitaifa, Ukur Yatani amependekeza bajeti ya hazina ya Michezo, Sanaa na Maendeleo ya Jamii kuwa Sh15.8 bilioni katika mwaka wa fedha ujao.

Katika hotuba yake ya bajeti bungeni mnamo Alhamisi, Waziri Yatani ameongeza mgao wa hazina hiyo kwa asilimia 5.3 kutoka ile ya mwaka uliopita.

Mwaka uliopita, Yatani alipendekeza kutengea hazina hiyo Sh15 bilioni, nyongeza ya Sh1 bilioni kutoka mwaka wa fedha wa 2020/2021.

Yatani ameongeza mgao huo kutumiwa katika kukarabati viwanja vya kimaeneo kwa asilimia 38.8 kutoka Sh90 milioni mwaka jana hadi Sh125 milioni mwaka huu.

Miongoni mwa viwanja vinavyoendelea kujengwa ama vimekuwa vikikarabatiwa tangu 2017 na serikali imeshatumia zaidi ya Sh1 bilioni ni Kipchoge Keino katika kaunti ya Uasin Gishu, Kamariny (Elgeyo Marakwet) na Ruring’u (Nyeri).

Pia, kuna uwanja wa Wote katika kaunti ya Makueni na Kinoru katika kaunti ya Meru.

Mnamo Machi 26, Rais Uhuru Kenyatta alifungua kituo cha michezo cha Jamhuri kilichokarabatiwa jijini Nairobi. Ukarabati, ambao ulianza Agosti 6, 2020, ulifanywa na kampuni ya M.S. Dallo Holdings Limited kwa gharama ya Sh609 milioni.

Kituo cha Jamhuri kina viwanja vitatu vya soka na uwanja mmoja wa raga pia sehemu ya kukimbilia ya kilomita 3.7, vyoo, vyumba vya kubadilishia mavazi, sehemu mbili za kujistarehesha na sehemu ya watoto kucheza.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Walimu roho mkononi TSC ikiwahamisha

Serikali ya Trans-Nzoia yalaumiwa kwa ukosefu wa dawa...

T L