• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
AG aanza rasmi juhudi za kuokoa BBI

AG aanza rasmi juhudi za kuokoa BBI

Na JOSEPH WANGUI

Mwanasheria Mkuu, Paul Kihara Kariuki hatimaye amewasilisha rasmi rufaa katika Mahakama ya Juu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ulioharamisha mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia Mpango wa Maridhiano (BBI).

Katika rufaa yake, Mwanasheria Mkuu anataka Mahakama ya Juu kuamua masuala 11 ambayo yanaweza kufufua mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia BBI.

Miongoni mwa masuala hayo ni iwapo katiba inamzuia Rais kuunga mpango wa kubadilisha katiba.Anataka mahakama kuamua iwapo idara ya serikali, afisa wa serikali au mtumishi wa umma anaweza kuanzisha mabadiliko ya katiba kupitia mpango unaoungwa na raia.

Anataka Mahakama kuamua iwapo suala la muundo wa kimsingi wa katiba linatumika Kenya na iwapo unaweka mipaka ua kubadilisha katiba kulingana na ibara za 255 na 257.

Mwanasheria Mkuu hakuridhishwa na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kwamba katiba ya Kenya ina msingi ambayo unaweza kubadilishwa kupitia mfumo unaohusisha nguvu za raia.

Vile vile anataka mahakama iamue iwapo sehemu ya Mswada wa Kubadilisha Katiba wa 2020, yaani Mswada wa BBI, inakiuka katiba.Ni sehemu hii ya pili inayobuni maeneo bunge 70 katika kaunti 28.

You can share this post!

Kiangazi: Serikali yaahidi kununua mifugo

Rashford arejelea mazoezi baada ya kufanyiwa upasuaji...