• Nairobi
  • Last Updated May 16th, 2024 8:50 PM
Aibu yamvaa Mandago wakazi wakimuita mwizi

Aibu yamvaa Mandago wakazi wakimuita mwizi

NA TITUS OMINDE

SENETA wa Uasin Gishu Jackson Mandago hakuamini alichokiona baada ya wakazi kumuita “mwizi shujaa” alipojaribu kuwahutubia mnamo Ijumaa.

Wakazi wenye hamaki walianza kumnyooshea kidole cha lawama wakimuita mwizi alipojaribu kuahutubia akiwa kwenye msafara wa Naibu Rais Rigathi Gachagua wakati wakielekea katika uwanja wa Eldoret Sports Club kufunga Kongamano la Ugatuzi.

Wakazi hao walimwambia Mandago peupe kuwa yeye ni ‘mwizi stadi’ na wala si shujaa wa maendeleo.

Juhudi za kutumia ushujaa na ulumbi wake kuwahutubia wananchi katika barabara ya Oginga Odinga karibu na mkahawa maarufu wa Members, ziligonga mwamba huku wimbo “mwizi… mwizi” ukisheheni.

Bw Mandago aliaibika akakimbilia usalama ndani ya gari lake baada ya makelele kuzidi.

Umati uliojawa na hasira uliendela kumkejeli kwa lugha chafu kwa kukerwa naye kufuatia sakata ya wizi wa Sh1.1 bilioni za wazazi waliotaka watoto wao waende nchini Finland na Canada kwa masomo ya juu.

“Hatutaki utuhutubie. Ondoka hapa hatutakusikiliza,” akasikika mmoja wa wakazi waliokuwa sehemu ya umati huo.

Dereva wa gari la seneta huyo alishika usukani kisawasawa akaondoka hapo upesi.

Sakata hiyo ilisukwa wakati alikuwa Gavana wa Kaunti ya Uasin Gishu.

Alifokewa kipindi cha saa 24 tu baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 katika Mahakama ya Nakuru aliposhtakiwa Alhamisi.

Bw Mandago alikamatwa Jumatano pamoja na wenzake wawili wakafikishwa mahakamani, Alhamisi, Agosti 17, 2023 kusomewa mashtaka kuhusiana na kashfa hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Gachagua kwa Odinga: Wewe ni raia binafsi asiyeweza hata...

Tanzia: Watu 6 wafariki asubuhi ya harusi

T L