• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Gachagua kwa Odinga: Wewe ni raia binafsi asiyeweza hata kutoa amri ya uhamisho wa chifu 

Gachagua kwa Odinga: Wewe ni raia binafsi asiyeweza hata kutoa amri ya uhamisho wa chifu 

NA SAMMY WAWERU 

NAIBU wa Rais Rigathi Gachagua amemsuta kinara wa upinzani, Raila Odinga akimtaja kama ‘raia binafsi asiye na mamlaka ndani ya serikali’. 

Bw Gachagua aliendeleza mashambulizi yake kwa Bw Raila, kufuatia matamshi yake ambapo alimtaka Balozi wa Amerika hapa Kenya, Bi Meg Whitman kukoma kuingilia masuala ya humu nchini.

Akirejelea uchaguzi mkuu wa 2022, Bi Meg alisema zoezi hilo lilikuwa la huru, haki na uwazi hivyo basi Rais wa sasa William Ruto ni halali.

Matamshi hayo, hata hivyo, yalionekana kukera Bw Raila ambaye alimenyana na Dkt Ruto.

Kiongozi huyo wa Azimio la Umoja, akimjibu Balozi Meg, alimtaka kukoma kuingilia masuala ya ndani kwa ndani Kenya.

Bw Gachagua, alikuwa mwepesi wa kumjibu Raila Odinga sawa na Rais Kenyatta, akisema yeye (Raila) ni raia binafsi asiye na usemi wowote katika serikali ya Kenya Kwanza.

“Tunapaswa kuheshimu wawekezaji wetu…Wewe (akiashiria Raila Odinga) ni raia binafsi asiye hata na mamlaka kutoa amri chifu ahamishwe,” Gachagua alimkashifu.

Naibu Rais alitoa kauli hiyo mnamo Ijumaa, Agosti 18, 2023 akihutubu wakati wa kufunga rasmi Kongamano la Ugatuzi 2023, lililofanyika Eldoret, Uasin Gishu.

Bw Raila pia alisuta Balozi Meg, akihutubia kongamano hilo.

Waziri Mkuu huyo wa zamani ni kati ya viongozi na wanasiasa mashuhuri waliotetea kupitishwa kwa Katiba ya sasa 2010.

Serikali za ugatuzi zilianzishwa 2013.

Akimshambulia kiongozi wa upinzani, Bw Gachagua alisema hana mamlaka yoyote kuamuru Bi Meg aondolewe nchini.

“Balozi Meg Whitman alishambuliwa bila makosa yoyote. Ninamhimiza apuuzilie mbali madai ya Raila Odinga.”

 

  • Tags

You can share this post!

Bodaboda waliotafuta petroli ya magendo wauziwa mkorogo wa...

Aibu yamvaa Mandago wakazi wakimuita mwizi

T L