• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Anne Nderitu akataa vyama vinavyofanana na ODM

Anne Nderitu akataa vyama vinavyofanana na ODM

NA CHARLES WASONGA

MSAJILI wa Vyama vya Kisiasa Anne Nderitu amekataa ombi kutoka kwa Mkenya mmoja ambaye alitaka afisi yake ihifadhi majina matatu yanayofanana na ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM).

Katika barua aliyomtumia Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna, Nderitu alikataa kuhifadhi majina; ODM Asili, ODM Kamili na ODM Mpya yaliyowasilishwa kwa afisi yake na aliyekuwa Waziri wa Barabara na Ujenzi katika Kaunti ya Kisumu Thomas Owiti.

“Afisi hii imekataa ombi la kuhifadhi majina ya vyama yaliyopendekezwa kwa sababu hayakutimiza matakwa ya Sehemu ya 8 ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa, 2022,” ikasema barua ya Bi Nderitu aliyomwandikia Bw Sifuna.

Katika barua aliyomwandikia msajili huyo wa vyama vya kisiasa mnamo Machi 13, 2023, Bw Owiti aliomba afisi hiyo ihifadhima majina ya; ODM Asili, ODM Kamili na ODM Mpya kwa ajili ya kusajiliwa rasmi kuwa vyama vya kisiasa.

Lakini katika barua ya pamoja kwa afisi ya Bi Nderitu mwenyekiti wa ODM John Mbadi na Katibu Mkuu Bw Sifuna walipinga pendekezo hilo wakimtaka akatae ombi hilo.

“Ombi hilo linakiuka matakwa ya Sehemu ya 8 ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa. Aidha, ombi hilo lina malengo malengo mabaya kwa linalenga kuwakanganya wanachama wetu na umma kwa ujumla kuhusu utendakazi wa chama chetu,” Mbw Mbadi na Sifuna wakasema.

Kulingana na Sehemu ya 8 ya Sheria hiyo mtu anayewasilisha ombi la kutaka kusajili chama cha kisiasa anafaa kuhakikisha kuwa jina analolipendekeza halifanani kwa njia zozote na chama au vyama ambavyo tayari vimesajiliwa.

Chama cha ODM kilibuniwa mnamo Novemba 2005 baada ya kura ya maamuzi kuhusu Katiba Mpya ambapo kundi la LA ambalo alama ya ilikuwa Chungwa, liliibuka mshindi.

Kundi hilo liliongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga na wanasiasa wengine kama vile aliyekuwa Makamu wa Rais Moody Awori, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Kanu marehemu J J Kamotho, aliyekuwa Waziri wa Utalii Najib Balala, miongoni mwa wengine.

  • Tags

You can share this post!

Tuongeze ukarimu wetu kumi la rehema likimalizika

Mjumbe wa handisheki atua Kenya

T L