• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Jubilee inanidhulumu, alia mwaniaji ubunge Kabuchai

Jubilee inanidhulumu, alia mwaniaji ubunge Kabuchai

Na Brian Ojamaa

MWANIAJI aliyeazimia kugombea kiti cha eneobunge la Kabuchai kwa tiketi ya chama cha Jubilee, amelalamikia uamuzi wa chama hicho kujiondoa kwenye uchaguzi huo na kuunga mgombeaji wa chama cha Ford Kenya.

Akiongea wa wanahabari mjini Bungoma, Dkt Evans Makokha alisema chama hicho kilikosea kwa kujiondoa katika uchaguzi huo.

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju wiki jana alisema kwamba chama hicho hakitawasilisha wagombeaji katika chaguzi ndogo maeneobunge ya Matungu, Kabuchai na useneta kaunti ya Machakos.

Bw Tuju alisema uamuzi huo uliafikiwa ili kudhihirisha msimamo wa chama wa kuunganisha nchi kupitia Mpango wa Maridhiano.

Hata hivyo, Bw Makokha alishangaa kwa nini chama hicho kilikubali kupokea ada ya Sh100,000 ya uteuzi na hata kuwasilisha jina lake kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inavyohitajika kisheria na kisha kubadilisha nia baadaye.

Alisema uamuzi huo unamaanisha hana muda kuhamia chama kingine.Makokha alisema alipokea simu kutoka kwa Bw Tuju akihudhuria mkutano na maafisa wa IEBC akiwa na wawaniaji wengine kumfahamisha chama kilikuwa kimeondoa jina lake.

 

You can share this post!

Ulinzi mkali mmoja akinaswa akiwa na bastola, risasi 500...

Museveni aahidi kujali zaidi maslahi ya maskini