• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:44 PM
Kajwang’ amshauri Wanjigi akubali kuunga mkono Raila

Kajwang’ amshauri Wanjigi akubali kuunga mkono Raila

NA GEORGE ODIWUOR

SENETA wa Homa bay Moses Kajwang’ amemshutumu mfanyabiashara Jimi Wanjigi kwa madai ya kudhoofisha chama cha ODM kwa kuomba kura kutoka eneo la Nyanza.

Hii ni baada ya Bw Wanjigi kutawazwa kama mzee wa jamii ya Waluo wiki iliyopita, hatua iliyompa fursa ya kuzunguka huru Nyanza akisaka uungwaji mkono.

Seneta huyo amesema kuwa Bw Wanjigi hajafuzu kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya ODM kwa sababu sheria za chama zinamzuia kufanya hivyo.

Badala yake, Bw Kajwang anamtaka mfanyabiashara huyo kuunga mkono azma ya urais ya kiongozi wa ODM, Raila Odinga na akome kujaribu kuyumbisha chama hicho katika eneo la Nyanza.

Bw Wanjigi alitawazwa mzee wa jamii katika hafla iliyofanyika eneobunge la Kabondo Kasipul, ambapo alitangaza atakuwa na misururu ya kampeni Homa Bay, Siaya, Migori na Kisumu yanayochukuliwa ngome ya kisiasa ya Raila Odinga.

Kulingana na mfanyabiashara huyo, anazo suluhisho bora zaidi kwa matatizo yanayowakumba wakazi eneo hilo na hivyo basi anastahili kuteuliwa kupeperusha tiketi ya ODM.

Alimtaka Bw Odinga kustaafu siasa na kumpisha aongoze ODM.

“Tunamtakia kila la kheri kwa sababu kila mtu ana haki ya kuwania nafasi ya uongozi chamani. Lakini nafasi ya mpeperushaji bendera katika ODM imehifadhiwa kiongozi wa chama,” alisema.

You can share this post!

ICC: Gicheru apumua ombi la upande wa mashtaka likitupwa nje

TAHARIRI: Tuwachuje wanasiasa kwa makini mara hii

T L