• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Kundi la Wabunge wa Pwani lapata viongozi wapya

Kundi la Wabunge wa Pwani lapata viongozi wapya

NA CHARLES WASONGA

MBUNGE wa Wundanyi Danson Mwashako ndiye mwenyekiti mpya wa Kundi la Wabunge wa Pwani (CPG).

Bw Mwashako ambaye alichaguliwa Jumatano, sasa amejaza nafasi iliyoachwa wazi na mwenyekiti wa zamani marehemu Suleiman Dori (aliyekuwa Mbunge wa Msambweni) aliyefariki mnamo Machi 10, 2023.

Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kilifi Getrude Mbeyu ndiye alichaguliwa naibu mwenyekiti huku Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu.

Kiti cha Mwekahazina nacho kilimwendea Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Tana River Amina Dika, ambaye atasaidiana na Seneta wa Lamu Joseph Githuku kama naibu wake.

Mbungu wa Garsen Ali Wario alichaguliwa kuwa Katibu mpanga ratiba na naibu wake atahudumu Mbunge wa Mvita Masoud Machele anayehudumu muhula wa kwanza bungeni.

Nao wadhifa wa Kiranja wa kundi hilo la CPG, ulimwenda Mbunge wa Kilifi Kusini Ken Chonga, anayehudumu muhula wa pili.

Wabunge hao walikubaliana kwa kauli moja kwamba Naibu Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa Owen Baya Yaa, ambaye ni Mbunge wa Kilifi Kaskazini, ahudumu kama Mdhamini wa CPG.

Muungano huo wa wabunge wa Pwani pia ulibuni muungano wa wabunge wanawake (Women Caucus). Mbunge wa Lamu Mashariki Kapteni Ruweida Mohamed Obbo, ndiye aliyechaguliwa kuwa mwenyekiti.

  • Tags

You can share this post!

Vihiga Queens kuanza dhidi ya Ulinzi Starlets msimu mpya wa...

Rais Ruto atarajiwa kuzindua miradi ya maendeleo eneo la...

T L