• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 11:13 AM
Makundi mbalimbali yataka Ruto, Raila waingie muafaka

Makundi mbalimbali yataka Ruto, Raila waingie muafaka

NA JUSTUS OCHIENG

RAIS William Ruto na kinara wa Azimio la Umoja, Raila Odinga, wako kwenye shinikizo kubuni Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kurejesha uthabiti wa kisiasa nchini.

Taifa Leo’ imebaini kuwa juhudi za kuwarai wawili hao kubuni handisheki kama ile iliyobuniwa 2018 baina ya Bw Odinga na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta zinaendelea kushika kasi.

Mwafaka baina ya viongozi hao ulifuatia utata uliozuka kuhusu uchaguzi wa urais wa 2017.

Duru katika kambi za Rais Ruto na Bw Odinga ziliiambia ‘Taifa Leo’ kwamba katika kumaliza mzozo huo, huenda kukawa na suluhisho mbili—kubuniwa kwa Afisi ya Kiongozi Rasmi wa Upinzani au kubuniwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Rais Ruto amelazimika kujitokeza hadharani kushinikiza kubuniwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani kupitia Bunge la Kitaifa ili kumfaa Bw Odinga. Lengo kuu la hili ni kumaliza mzozo huo na kuepuka hali ambapo huenda upinzani ukajumuishwa katika serikali yake.

‘Taifa Leo’ imebaini kuwa mapendekezo hayo yaliibuka wakati wa mazungumzo yaliyoongozwa na mwakilishi wa Rais Joe Biden wa Amerika—Seneta Chris Coons wa Delaware—aliyeondoka nchini wiki mbili zilizopita na viongozi wa Kanisa Katoliki waliokutana na Bw Odinga.

Ni kutokana na hilo ambapo wakati wa hotuba yake kwa taifa mnamo Aprili 2, Rais Ruto alieleza kujitolea kwake katika kubuniwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani kupitia mchakato wa bunge, pendekezo ambalo Bw Odinga amekataa kabisa.

  • Tags

You can share this post!

Taita Taveta: Maafisa wachunguzwa kufuja Sh4m hafla ya Vita...

Rais azuru kaunti yake ghafla kwa sikukuu ya Pasaka

T L