• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 6:55 AM
Masanduku yenye kura yaanza kutua kituo kikuu cha kuhesabia Kieni

Masanduku yenye kura yaanza kutua kituo kikuu cha kuhesabia Kieni

NA SAMMY WAWERU
 
MAAFISA wa IEBC, maajenti wa vyama vya kisiasa na wa wagombea wa viti vya kisiasa chini ya ulinzi wa maafisa wa polisi wameanza kuwasilisha masunduku yenye kura katika kituo kikuu cha kujumuisha eneobunge la Kieni, Nyeri.
 
Masanduku hayo aidha yanatoka vituo mbalimbali vya kupigia kura.
 
Foleni ndefu zinashuhudiwa katika kituo hicho, kilichoko Shule ya Upili ya Mweiga.
 
Shughuli ya kuwasilisha masanduku ilianza mwendo wa saa nane usiku, maafisa husika wakivumilia kijibaridi kikali cha asubuhi eneo hilo.
 
Unyevuunyevu unashuhudiwa Mweiga, ikizingatiwa kuwa eneo hilo linakaribia Mlima Kenya.
 
Mmoja wa maafisa rejeshi wa IEBC Kieni, anaendelea kutangaza matokeo ya kura kutoka vituo mbalimbali.
 
Anasoma ya viti vyote sita; urais, gavana, seneta, mbunge, mwakilishi wa wanawake na diwani (MCA).
 
Hata hivyo hayajajumuishwa, kutambua walioibuka washindi katika viti hivyo vya kisiasa.
  • Tags

You can share this post!

Wapiga kura 10 milioni wakosa kufika vituoni

Wagombea waanza kuvuna walichopanda kipindi cha kampeni

T L