• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mbunge aomba msaada wa Rais kusaidia wahasiriwa wa mkasa wa ajali ya mafuta Gem

Mbunge aomba msaada wa Rais kusaidia wahasiriwa wa mkasa wa ajali ya mafuta Gem

Na SAMMY WAWERU

Mbunge wa Gem Elisha Odhiambo amemsihi Rais Uhuru Kenyatta kuungana na viongozi wa Siaya kusaidia familia za waathiriwa wa mkasa wa ajali ya mafuta Siaya.

Jumapili, lori lililokuwa likisafirisha mafuta lilianguka eneo la Gem, katika barabara kuu ya Kisumu – Busia, na kusababisha maafa ya watu waliojitokeza kuteka mafuta.Watu 14 wamethibitishwa kufariki na 25 kupata marejaha mabaya, kufuatia ndimi za moto uliotokea.

“Ninamhimiza Rais Uhuru Kenyatta aungane nasi katika kusaidia kuzika waliofariki, waliopata majeraha na familia za wahasiriwa,” akasema Bw Odhiambo.Kulingana na mbunge huyu, kuna miili ya baadhi ya waathiriwa iliyoteketea kiasi cha kutoweza kutambulika.

“Hii ina maana kuwa tutahitaji kufanya uchunguzi wa chembechembe za msimbojeni,” akaelezea.Kwa upande wake seneta wa Siaya, Bw James Orengo, alisema serikali ya kaunti hiyo itafanya kila iwezalo kuhakikisha familia za wahasiriwa zinaweza kuzika wapendwa wao.

“Tayari tumezindua kituo cha utoaji nasaha na ushauri kwa familia za waathiriwa,” seneta Orengo akasema.Visa vya watu kufizia mafuta ya petroli, lori za kuyasafirisha zinapoanguka si vigeni nchini.

Endapo tukio kama hilo linafanyika, unatahadharishwa na kutakiwa kutokuwa katika mazingira ya mkasa wa aina hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Rangers kukutana na Malmo au HJK Helsinki katika mchujo wa...

Odinga aitaka idara ya polisi na mahakama kufanya hima...