• Nairobi
  • Last Updated December 2nd, 2023 1:45 PM
Mbunge atumai Gideon Moi atanyaka tiketi ya OKA

Mbunge atumai Gideon Moi atanyaka tiketi ya OKA

Na KNA

 

MBUNGE wa Tiaty, Bw William Kamket, ana matumaini kwamba kinara wa chama cha KANU, Seneta Gideon Moi wa Baringo, huenda akanyakua tiketi ya kugombea urais ya One Kenya Alliance (OKA).

Akizungumza Jumatatu wakati wa usajili wa wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo ya Matibabu Kenya (KMTC) bewa la Chemolingot mjini Baringo, Bw Kamket alisema kinara huyo ana sifa za kutosha kuwania urais.

Tiketi hiyo ya OKA pia inamezewa mate na vinara wengine wa muungano ikiwemo Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper) na Moses Wetangula wa Ford Kenya.

You can share this post!

Kiraitu, Munya wafufua uhasama kuelekea 2022

TAHARIRI: TSC idhibiti zogo la shule haraka