• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Muturi azindua rasmi azma ya urais, akataa miungano kabla ya uchaguzi

Muturi azindua rasmi azma ya urais, akataa miungano kabla ya uchaguzi

Na WANDERI KAMAU

SPIKA wa Bunge la Kitaifa, Bw Justin Muturi, Jumapili alizindua rasmi azma yake ya kuwania urais hapo Agosti kwa tiketi ya chama cha Democratic Party (DP).

Bw Muturi alizindua azma yake wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wajumbe (NDC) wa chama lililofanyika katika Ukumbi wa Bomas, jijini Nairobi.

Kwenye hotuba yake, Bw Muturi alisisitiza kuwa atakuwa debeni kwenye kinyang’anyiro hicho na hataingia kwenye muungano wowote wa kisiasa.

“Nitakuwa debeni kama wagombea wengine. Sitakubali dhana inayoendeshwa kuwa kinyang’anyiro hicho ni kati ya wagombea wawili tu. Tunapoanza safari hii, msimamo wangu ni kuwa tutaenda kivyetu bila kuingia kwenye muungano wowote wa kisiasa. Tutafanya hivyo baada ya uchaguzi kukamilika kulingana na mazingira ya kisiasa yatakavyokuwa,” akasema Bw Muturi.

Kauli yake inaonekana kuvuruga karata za kuliunganisha eneo la Mlima Kenya, ambazo zimekuwa zikiendeshwa na viongozi kama Martha Karua (Narc-Kenya), Moses Kuria (Chama Cha Kazi) na Mwangi Kiunjuri (The Service Party-TSP) chini ya vuguvugu la Mt Kenya Unity Forum (MUF).

Viongozi hao wamekuwa wakisisitiza kuwa eneo hilo linapaswa kuwa na sauti moja ya kisiasa. ikizingatiwa halitakuwa na mgombea-urais kwenye uchaguzi wa Agosti.

Hata hivyo, Bw Muturi alisisitiza yeye si kiongozi wa kikanda bali wa kitaifa, akitaja hilo kama sababu kuu ya kutafuta urais.

  • Tags

You can share this post!

Man-United wakomoa Leeds United baada ya kuponea ugani...

Johnson adai Urusi inapanga kuzua vita vikubwa Ulaya

T L