• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 7:52 PM
Paul ‘Mamba’ Chebor ang’oa Moi katika eneobunge la Rongai

Paul ‘Mamba’ Chebor ang’oa Moi katika eneobunge la Rongai

NA FRANCIS MUREITHI

RAYMOND Kipruto Moi ameshindwa kuhifadhi kiti cha eneobunge la Rongai baada ya kulemewa na mgombea wa United Democratic Alliance (UDA) Paul ” Mamba” Chebor aliyejizolea 27,021.

Uchaguzi katika eneo hilo ulifanyika jana Jumatatu, Agosti 29, 2022.

Raymond amekuwa wa pili kwa kupata kura 14,725 huku Luka Kigen wa Chama Cha Mashinani (CCM) akifaulu kupata kura 593 pekee.

Idadi jumla ya waliojisajili kupiga kura ilikuwa ni 84,625.

Ni uchaguzi ulioleta ushindani mkali kati ya mrengo wa familia ya aliyekuwa Rais wa Pili marehemu Daniel Toroitich Arap Moi na Rais Mteule wa uchaguzi wa Agosti 9, 2022 Dkt William Ruto wa UDA.

Mara baada ya kutangazwa mshindi, Bw Chebor ametoa hotuba ya kuwapongeza wakazi wa Rongai, Kaunti ya Nakuru.

“Ninawapongeza wakazi wa Ringai kwa kuniamini na kunipa kura. Ninaahidi kwamba sitawaangusha. Nitashirikiana na kila mkazi bila kubagua aliyenichagua au aliyeninyima kura,” akasema Bw Chebor.

Kituo cha kujumlisha kura kilikuwa ni Chuo cha Mafunzo ya Ualimu Nakuru.

Uchaguzi wa 2022 umekuwa kama dhoruba kali lililosomba familia ya Moi baada ya Gideon Moi kubwagwa na William Cheptumo wa UDA ambaye sasa ni seneta mteule wa Baringo.

  • Tags

You can share this post!

Magavana waanza kazi kwa kishindo

Nottingham Forest wasajili beki mzoefu, Renan Lodi, kutoka...

T L