• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:50 AM
Ruto aahidi kuwalainishia Wakenya maisha akichaguliwa rais

Ruto aahidi kuwalainishia Wakenya maisha akichaguliwa rais

NA SAMMY WAWERU

NAIBU Rais Dkt William Ruto sasa anadai mfumo wa ugavi wa raslimali wa ‘shilingi moja kwa mtu mmoja mmoja’ uliopendekezwa kwenye Mswada wa Ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI), ulikuwa wazo la vuguvugu la Hasla.

Mswada huo uliokuwa ukipendekeza mabadiliko ya Katiba, hata hivyo, mahakama iliamua mnamo Machi 2022 kwamba utaratibu uliotumika kuusukuma ulikiuka Katiba.

Korti ilihoji, waasisi ambao ni Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga hawakufuata sheria kuanzisha mswada huo maarufu.

“Mfumo wa ugavi wa raslimali wa shilingi moja kwa mpiga kura mmoja, ulikuwa wazo la hastla,” Dkt Ruto akasema.

Naibu rais amekuwa akitumia kauli ya hastla kufanya kampeni kuingia Ikulu, nembo inayohusishwa na wananchi wa mapato ya chini.

Alisema hayo Jumapili, akihutubia taifa nyumbani kwake Karen, jijini Nairobi katika kikao cha muungano wa Kenya Kwanza ambapo alitangaza mbunge wa Mathira, Bw Rigathi Gachagua atakuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu ujao, Agorti 9, 2022.

Ruto ndiye atapeperusha bendera ya urais ya muungano huo kwenye uchaguzi.

“Tutatathmini mfumo wa ukusanyaji ushuru ili kupunguza gharama ya maisha inayoendelea kulemea Wakenya,” naibu rais akaelezea.

“Isitoshe, mfumo wa serikali ya Kenya Kwanza (endapo itafanikiwa kumrithi Rais Kenyatta) katika kutoza ushuru utalenga kuondoa mikopo na kufanya maendeleo,” akasema.

Uchaguzi ujao, Dkt Ruto na kiongozi wa ODM, wametajwa kuwa wagombea wakuu kufuatia umaarufu wao nchini.

  • Tags

You can share this post!

UDA: Ni tiketi ya Ruto-Gachagua

Liverpool wazamisha Chelsea na kutwaa Kombe la FA kwa mara...

T L