• Nairobi
  • Last Updated April 12th, 2024 4:55 PM
Ruto ni maarufu kuliko raila eneo la Mlimani’

Ruto ni maarufu kuliko raila eneo la Mlimani’

Na JUSTUS WANGA

GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la Mlima Kenya kutokana na ziara zake za kila mara eneo hilo.

Kwenye mahojiano ya kipekee na “Taifa Jumapili” Bw Murungi alisema Dkt Ruto amezuru kaunti ya Meru pekee mara 53 na hivyo anajulikana hadi ngazi za vijijini.“Tangu uchaguzi mkuu wa 2013, Ruto amezuru Meru zaidi ya mara 53 akitembelea makanisa na hata vijijini.

Vile vile, amefaulu kuvutia idadi kubwa ya wabunge na madiwani upande wake hali inayomfanya kutambulika zaidi akilinganishwa na wagombeaji wengine wa urais,” Gavana Murungi akaeleza.Hata hivyo, alisema mjadala mkali sasa unaendelea katika eneo la Mlima Kenya kuhusu nani kati ya Dkt Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga anafaa kuungwa mkono kwa wadhifa wa urais.

“Hii ni kwa sababu tunaamini kwamba rais wa Kenya hafai kutoka eneo la Mlima Kenya kwa kipindi cha miaka 10. Rais wa tano wa Kenya hafai kutoka eneo letu,” Bw Murungi akasema.Alisema watu wa Mlima Kenya wanatafakari ikiwa huenda tunarejea katika enzi ambapo marehemu Daniel Moi ambapo eneo hilo lilitengwa.“

Hizo ni nyakati ambapo umasiki ulithiri, wakati ambapo sekta ya kahawa iliporomoka na wakazi wengi walishindwa kumudu karo ya watoto,” akasema. “Hata hivyo, binafsi ninamuunga mkono Raila kwa sababu ninataka rasilimali nyingi zaidi ziletwe katika kaunti yetu.

Siwezi kuomba maendeleo,” Bw Murungi akasema.Gavana huyo hata hivyo alikiri kuwa Ruto anasisimua vijana na raia wa tabaka la chini, maarufu kama hasla.“Hata hivyo, bado tunasikiliza. Kwa mfano, tunataka kujua mipango yake kwa watu wetu haswa katika nyanja ya kilimo,” Bw Murungi akasema.

You can share this post!

Rais azindua rasmi sanamu ya Ronald Ngala

Jamhuri ya mwisho ya Uhuru

T L