• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Rais azindua rasmi sanamu ya Ronald Ngala

Rais azindua rasmi sanamu ya Ronald Ngala

Na WINNIE ONYANDO

RAIS Uhuru Kenyatta jana alifungua rasmi sanamu iliyojengwa kwa heshima ya aliyekuwa Waziri na aliyepigania uhuru wa Kenya, Ronald Gideon Ngala(pichani), Kaunti ya Nairobi.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rais Kenyatta alisema kuwa serikali itaendelea kuwapa heshima viongozi mbalimbali waliopigania uhuru na kujenga uchumi wa nchi.“Kulingana na sheria inayowatambua mashujaa na waliofanya juhudi kujenga nchi, sasa nchi itawakumbuka na kuwasherehekea watu kama hao.

Hiyo itapitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine,” akasema Rais Kenyatta.Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na familia ya Bw Ronald Ngala wakiongozwa na aliyekuwa waziri serikalini, Noah Katana Ngala.Rais Kenyatta pia alitambua juhudi za kiongozi huyo mashuhuri aliyezindua filosofia ya ‘Majimbo’ jambo lililoleta mabadiliko nchini hadi sasa.

Kando na uzinduzi wa filosofia hiyo ya ‘Majimbo’, Bw Ngala pia anasherehekewa kwa kuwa katika kipaumbele katika uundaji wa katiba mpya, uzinduzi wa vyama mbalimbali na kwa bidii zake katika ujenzi wa uchumu.“Bw Ngala alijiwajibika sana katika kazi yake.

Aliwahimiza watu kutia bidii na kuangalia maisha ya baadaye kupitia kauli mbiu yake ya ‘Jeza Zhomu, Lenga Dzulu’, inayojulikana kama ‘Tia bidii na ulenga maisha ya baadaye.”Hata hivyo, Rais Kenyatta aliipongeza Wizara ya Michezo, Utamaduni na Turathi kwa kuendelea kutunza na kudumisha sanamu za mashujaa kote nchini, huku akitaja mifano ya sanamu za Dedan Kimathi jijini Nairobi na Paul Ngei Kaunti ya Machakos.

You can share this post!

Wapwani kweli wataungana kisiasa au ni ndoto ya mchana?

Ruto ni maarufu kuliko raila eneo la Mlimani’

T L