• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Tuungane tulinde maslahi ya Mlima Kenya – Kiunjuri

Tuungane tulinde maslahi ya Mlima Kenya – Kiunjuri

Na Alex Njeru

KIONGOZI wa Chama cha TSP amewataka viongozi wa Tangatanga na Kieleweke waungane ili kuhakikisha maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya yanajumuishwa kwenye mchakato wa marekebisho ya katiba unaoendelea.

Bw Kiunjuri alisema mgawanyiko unaoendelea kushuhudiwa kati ya viongozi hao ni hatari na huenda ukasababisha waelekee upinzani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Waziri huyo aliitaka mirengo hiyo miwili ambayo inaunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kwa upande moja na Naibu Rais Dkt William Ruto kwa upande mwingine, izungumze kwa sauti moja kabla ya kuamua mgombeaji watakayempigia kura 2022.

Dkt Ruto, Kinara wa ODM Raila Odinga na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, ni kati ya viongozi ambao wananyemelea kura za Mlima Kenya wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta atastaafu siasa mwaka ujao.‘Kwa minajili ya maslahi ya watu wetu, lazima tuungane na kuamua njia ya kufuata 2022.

Tunafaa tuhakikishe tunayemuunga mkono atazingatia maslahi yetu baada ya kuingia afisini,” akasema Bw Kiunjuri alipohudhuria hafla ya mazishi katika Kaunti ya Tharaka Nithi.

Mbunge huyo wa zamani wa Laikipia Mashariki alifichua kuwa yupo radhi kupatanisha pande zote mbili ili wahakikishe matakwa ya wakazi yanajumuishwa kwenye BBI aliyoitaja kama mradi wa serikali.

Mwanasiasa huyo alisema kuwa kuna viongozi kutoka maeneo mengine ambao hawajapendezwa na mfumo mpya wa kugawa mapato kwa kaunti na kubuniwa kwa maeneo bunge mapya huku eneo hilo likinufaika mno.

 

You can share this post!

Wakili kortini kwa madai ya kulaghai mayatima Sh100m

Kaunti yapewa siku 7 kujibu kesi ya wafanyabiashara