• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
UDA hatarini ‘kujikwaa’ kama Jubilee

UDA hatarini ‘kujikwaa’ kama Jubilee

JAMES MURIMI NA WANDERI KAMAU

RAIS William Ruto yuko kwenye hatari ya kurudia ‘kosa’ la mtangulizi wake, Uhuru Kenyatta, kupitia shinikizo zilizopo kwamba lazima vyama vyote washirika katika mrengo wa Kenya Kwanza vivunjwe na kujiunga na chama tawala, UDA.

Katibu Mkuu mpya wa UDA, Bw Cleophas Malala, amesisitiza kuwa lazima vyama vyote katika mrengo huo vivunjwe, ili kuhakikisha kuwa utashiriki kwenye uchaguzi wa 2027 kama chama kimoja.

Kando na UDA, vyama vingine washirika katika muungano huo ni Amani National Congress (ANC), Ford-Kenya, Democratic Party (DP), Pamoja African Alliance (PAA), Economic Freedom Party (EFP), The Service Party (TSP), Chama Cha Kazi (CCK) kati ya vingine.

“Lengo langu ni kuhakikisha Rais Ruto amechaguliwa tena kama rais 2027. Mpango uliopo ni kuhakikisha kuwa amepata idadi kubwa zaidi ya wabunge. Hali ilivyo, ni kama vyama hivyo vyote vimefutiliwa mbali,” akasema Bw Malala kwenye kikao na wanahabari Jumatatu.

Kulingana na Bw Malala, mkakati huo unamaanisha kuwa lazima Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula na mwenzake wa Seneti, Amason Kingi wajiuzulu kama viongozi wa vyama vya Ford-Kenya na PAA mtawalia.

Hata hivyo, tayari mkakati huo umeanza kupata pingamizi kali, hasa kutoka kwa uongozi wa vyama vya ANC na Ford-Kenya. Katika ANC, kiongozi wa chama hicho, Issa Timamy, amesisitiza kuwa chama hicho hakitavunjiliwa mbali.

“Ningetaka kuiweka wazi kuwa ANC haitavunjwa hata kidogo,” akasema Bw Timamy, ambaye ndiye gavana wa Lamu.

Hapo jana Jumanne, viongozi wa mrengo wa vijana katika chama cha Ford-Kenya, walimkosoa vikali Bw Malala, wakisema “anamdharau” Bw Wetang’ula kwa kumtaka kujiuzulu kama Spika.

“Tungetaka kumrai Bw Malala kukoma kumzungumzia Spika Wetang’ula kuwa lazima ajiuzulu nafasi yake kama Spika. Lazima amheshimu,” akasema Bw Evans Karani, ambaye ndiye kiongozi wa mrengo huo.

Gavana Mutahi Kahiga wa Nyeri, ambaye ni mshirika wa karibu wa Naibu Rais Rigathi Gachagua, alionya kuwa huenda Rais Ruto na Bw Gachagua wakajipata katika hali ambayo Bw Kenyatta alijipata 2017, kufuatia kuunganishwa kwa vyama tanzu vya muungano wa Jubilee.

“Tumeona kuwa kuna mipango ya kalainisha uongozi wa chama cha UDA. Tunamrai Rais wetu na naibu wake kuwa macho kwani tuna imani nao. Hata kama tunavunja vyama vingine katika muungano huo kubuni chama kimoja, lazima tuwe macho kutojipata pale tulikuwa katika chama cha Jubilee. Tunafaa kutosahau yale tuliyopitia,” akasema Bw Kahiga.

Akaongeza: “Nyote mnaweza kukumbuka vile viongozi wa Jubilee walivyoondolewa kama wezi, ilhali tulikuwa tumejitolea sana kukuza chama hicho. Asubuhi moja, tuliambiwa hatutakiwi.”

Kauli kama hiyo ilitolewa na mchanganuzi wa siasa Ngugi Njoroge, anayesema kuwa mivutano ambayo inafaa kuwafungua macho wawili hao.

  • Tags

You can share this post!

Madiwani waliumia miezi 6 ya 2022 bila marupurupu –...

Maandamano yachacha Nigeria kupinga matokeo

T L