• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 12:04 PM
Yathibitishwa gesi iliyopatikana Nyeri ni CO2

Yathibitishwa gesi iliyopatikana Nyeri ni CO2

Na BERNARDINE MUTANU

Gesi iliyopatikana wakati wa kuchimba kisima Nyeri ilikuwa dioksidi ya kaboni (CO2)kulingana na uchunguzi uliofanywa na kampuni ya Geothermal Development Company.

Huenda gesi hiyo ikaanza kuchimbwa, alisema afisa anayesimamia maji na rasilimali wa kaunti Bw Fredrick Kinyua.

Gesi hiyo ilipatikana katika kijiji cha Mwireri, katika eneo la Kieni. Huenda eneo hilo likajiunga na maeneo mengine kama vile Kereita, Kaunti ya Kiambu katika utoaji wa gesi ya dioksidi ya kaboni.

Mwaka jana, Kenya ilichimba gesi hiyo ya thamani ya Sh510 milioni kulingana na takwimu kutoka kwa Wizara ya Uchimbaji Madini.

Wachimbaji walipata gesi hiyo futi 250 ardhini na iliwabidi kusimamisha kazi yake kutokana na hilo.

You can share this post!

Watumizi wa mafuta taa nchini wapungua kwa 75%

Safaricom iliunda nafasi za ajira zaidi ya 800,000 –...

adminleo