• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 11:34 AM
Shule zafungwa Ivory Coast baada ya askari jela kulimana na wanachuo

Shule zafungwa Ivory Coast baada ya askari jela kulimana na wanachuo

CHARLES WASONGA Na MASHIRIKA

BOUAKE, Ivory Coast

SHULE kadha jijini hapa  zilifungwa Ijumaa kama hatua ya kupinga kisa ambapo askari wa gereza waliwashambulia wanafunzi katika bewa la chuo moja kikuu.

Wanafunzi wanane walijeruhiwa, watano kwa risasi, pale kundi la askari wa gereza waliposhambulio chuo hicho kwa risasi baada ya makabiliano kuzuka katika baa moja, afisa mkuu wa usalama mjini humo alisema.

Lakini chama cha wanafunzi chuo humo (CEECI) kilisema idadi ya wanafunzi waliojeruhiwa ni 11, kikisema baadhi ya wanafunzi walipigwa risasi huku wangine “wakikatwa kwa visu na mapanga”.

Askari wawili wa gereza la Bouake pia walijeruhiwa katika makabiliano hayo.

Kufuatia fujo hizo, viongozi wa chama hicho cha wanafunzi kilishurutisha kusitishwa kwa masomo katika shule mbili za upili na kadhaa za msingi, wakiwahimiza wanafunzi kuungana nao kulaani shumbulio hilo.

CEECI sasa inatoa wito kwa Serikali ya Ivory Coast kuhamisha gereza la Bouake pamoja na makazi ya askari wake ambayo yako mkabala na bewa hilo la Chuo Kikuu cha Alassane Ouattara magharibi mwa jijini hilo.

“Tumewaamuru wanafunzi wa shule za misngi na za upili kurejea nyumbani. Masomo yatarejelewa Jumatatu,” mwenyekiti wa CEECI Moustapha Ben Diamande alisema.

Wanafunzi na walioshuhudia walisema mapigano hayo ya Jumatano kati ya takriban wanafunzi 100 na askari 20, yalianza pale askari hao waliongia chuo na kuanza kufyatua risasi.

“Walikuwa na visu pamoja na mapanga.. ndipo tukaanza kuwarushia mawe,” mwanafunzi mmoja akaambia wanahabari wa AFP.

Duru kutoka pande mbili zilithibitisha kuwa kisa makabiliano hayo yalianza pale mwanafunzi mmoja alipozozana na askari mmoja katika baa moja.

You can share this post!

TAHARIRI: Wabunge wafahamu mswada hauepukiki

Dhuluma za kimapenzi dhidi ya wanawake zachacha Sudan Kusini

adminleo