• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 5:50 AM
Hofu Uganda wakazi wakizidi kutumia ARVs kugema mvinyo

Hofu Uganda wakazi wakizidi kutumia ARVs kugema mvinyo

NA MASHIRIKA

Kitgum, Uganda

WIZARA ya afya imeelezea wasiwasi wake kufuatia ongezeko la matumizi ya dawa ya kupunguza makali ya virusi vya HIV almaarufu Antiretroviral (ARVs) katika ugemaji wa pombe na kunenepesha nguruwe na kuku.

Kulingana na Wizara ya Afya ya Uganda, uharibifu huo wa dawa za ARVs umekithiri katika wilaya ya Kitgum.

Wakazi huchanganya vidonge vya ARVs na lishe ya mifugo kama vile nguruwe, ng’ombe, mbuzi na kuku kwa lengo la kutaka kuwawezesha kuwa wanene.

Kiongozi wa eneo la Mucwini Richard Komakech alisema kuwa dawa za ARVs zinatumiwa katika utengenezaji wa pombe na kupika maharagwe.

“Kulingana na wanaotumia vibaya dawa hiyo, vidonge vya ARV hufanya pombe kuchacha upesi na huivisha maharagwe kwa haraka,” akasema Komakech.

Alisema matumizi hayo mabovu ya vidonge vya ARVs ni changamoto katika vita dhidi ya Ukimwi.

Afisa wa Afya wa eneo hilo, Dkt Henry Okello Otto, alisema mbali na matumizi hayo kuwa haramu, vidonge vya ARVs vina madhara kwa afya ya watu wasiokuwa na virusi vya HIV mwilini.

You can share this post!

Watawa wakiri kuiba mamilioni na kuyatumia kucheza kamari

Mmoja auawa, washukiwa 10 wa genge hatari wakinaswa Mombasa

adminleo