• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 9:50 AM
GWIJI WA WIKI: Wadi Sandichi

GWIJI WA WIKI: Wadi Sandichi

Na CHRIS ADUNGO

YEYOTE mwenye ari ya kufanikiwa katika kile anachokifanya sharti ajitolee sabili, ajihini mengi, ajikusuru na awe mwepesi wa kujifunza kutoka kwa watangulizi wake.

Mtu msikivu siku zote huwa na hoja nzito, muhimu na zenye maana kila anapofungua kinywa chake kunena.

Ninawahimiza vijana wasiwe wepesi wa kukata tamaa kila wanapokabiliwa na changamoto maishani.

Wanastahili wawe wanyumbufu na wenye nia ya kushindana na wakati ili waimudu kasi ya mabadiliko ya jamii zao kitamaduni, kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia.

Wadi Sandichi. Picha/ Hisani

Ninawaomba sana wakereketwa, watetezi na wapenzi kindakindaki wa Kiswahili wasilegeze kamba katika juhudi zao za kuchangia maenezi na makuzi ya lugha hii.

Waendelee kuipigia chapuo na kuithamini vilivyo bila kusahau kwamba kichango ni kuchangizana.

Huu ndio ushauri wa Bw Godwin Wadi Sandichi – mwandishi mweledi wa Fasihi ya Kiswahili, mkufunzi stadi wa handiboli na mshairi shupavu ambaye kwa sasa ni Naibu Mwalimu Mkuu katika Shule ya Wavulana ya Kapsowar, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet.

Maisha ya awali

Bw Sandichi almaarufu Fakiri wa Maweni alizaliwa mnamo 1978 katika Kaunti ya Mombasa akiwa mtoto wa pili miongoni mwa watoto saba katika familia ya Mzee Yusuf Muyembe na Bi Antonina Muyembe.

Mzee Yusuf aliyekuwa mfanyakazi katika Wizara ya Mazingira alipopata uhamisho wa kuelekea Kitale, mwanawe Sandichi alisononeka si kidogo.

Huzuni yake ilichangiwa na ulazima wa kutengana ghafla na aliyekuwa mwalimu wake wa kwanza – baba mzazi aliyemlainisha vilivyo, kumpiga msasa, kumtia katika mkondo wa nidhamu kali na kumwandaa ipasavyo katika ulingo wa ushairi.

Hadi kufikia leo, haipingiki kwamba Mzee Yusuf alikuwa mtunzi mahiri sana wa mashairi, gwiji wa sanaa ya utani na mlumbi mpevu wa enzi yake!

You can share this post!

KAULI YA MATUNDURA: Furaha iliyoje kwamba sasa Uganda ina...

WASIA: Mashauriano ni muhimu kuwaadilisha vijana...

adminleo