• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
Kauli ya Mhubiri Lukas Ndung’u kuhusu misukosuko ya ndoa

Kauli ya Mhubiri Lukas Ndung’u kuhusu misukosuko ya ndoa

Na MWANGI MUIRURI

USHAWAHI kujiuliza ni kwa nini wanawake ndiYo hushawishika haraka kujiunga na dini na pia kuwa wakarimu maishani?

Na je, ushawahi kuwaza ni kwa nini wanaume ni wabaya sana katika biashara ambapo ukitaka kumtapeli utakumbana na ugumu?

Mhubiri Lukas Ndung’u akihubiri katika mazishi ya Hamuel Muguro Ngugi aliyeaga dunia Aprili 14 ndani ya kituo cha polisi cha Maragua
alikokuwa amezuiliwa baada ya kukamatwa katika mazingara tata, anakwambia sababu.

Mhubiri Lukas Ndung’u. Picha/ Mwangi Muiruri

Marehemu alizikwa katika kijiji cha Gathigia/Irembu katika Kaunti ndogo ya Maragua ndani ya Kaunti pana ya Murang’a.

Mhubiri Ndung’u anasema kuwa kwa kawaida, wanawake hawakimbizani na mengi kimaisha bali tu hupendezwa na kusemezwa vizuri na pia kuonyeshwa mapenzi.

“Wanaume mlio katika ndoa sasa pateni uhondo: Mwanamke utampa yote ya ulimwengu huu na bado akususie akimbizane na mwingine asiye na chochote cha kumpa ila tu maneno mazuri na matamu na yanayotolewa kwa heshima na upole wa hisia,” anasema.

Anasema kuwa hiki ndicho kiini cha wanawake wengi kutorokea makanisani na ambapo kila uchao unapata ndio wengi wanatapeliwa mitaani kwa kuwa “wahubiri huwasemeza vizuri, wanawaonyesha upendo na heshima na kisha kuwapa matumaini ya kesho katika imani ya kidini.”

Mhubiri Ndung’u wa Kanisa la Christian Foundation Church (CFF) lililoko Jijini Nairobi katika mitaa mbalimbali, yeye akiwajibikia tawi la Huruma anasema kuwa wanawake kwa kuwa ndio huzaa watoto huwa na mapenzi sana na kesho kuwaliko wanaume kwa kuwa “mwanamke huwa akiwazia neema ya hao watoto aliowazaa katika maisha yao ya kesho.”

Anasema kuwa hii ni kinyume na wanaume ambao raha yao sanasana katika uzazi ni “uhondo wa mzinga na asali kwa wakati huo na huwa wanawazia
kesho kwa msingi wa mzinga, asali na uhondo.”

Aliwataka wanaume; kama wangetaka kutiliwa maanani na wake zao, wajifunze adabu za kimsingi katika maongezi, wajifunze kuwa na heshima
na upole na cha mno, waanze kutilia maanani uthabiti wa kesho.

Wanawake wakishangilia eti walipendelewa katika ushauri huo, akawageuka ghafla na kuwapa mawaidha ya jinsi wao huchangia wanaume kutojali kesho, kutokuwa na adabu za kimaongezi na pia kukosa ile ladha ya mapenzi.

“Ukiwa hujui, mwanamume hapendi kupewa taswira ya suala lolote, bali hupenda kukumbana na hali hiyo ya suala, ana kwa ana,” akasema.

Aliongeza: “Kwa kuwa kuna watoto hapa, sitaki kuwa muwazi, lakini elewa hili; jiulize kama una akili timamu za kimapenzi ikiwa wewe
huingia katika kitanda chako cha ndoa kando ya mumeo ukiwa umevalia nguo za kampeni, za kukwea milima au zile ulitoka nazo kazini.”

Alisema kuwa “wanaume hupenjda kuonana ana kwa ana na hicho chake ulicho nacho mwilini mwako wala sio kupewa taswira eti kiko (kitu)
katika huo mwili lakini kuna mikakati ya kukiangaza nje kionekane ana kwa ana.”

Katika hali hiyo, alisema kuwa ndiyo sababu wanawake wengi hutorokea makanisani ili wakaongeleshwe vizuri na mapasta nao wanaume
wakitorokea kwenye hawafungiwi wanachohitaji bali wanapewa moja kwa moja waone kwa macho na waguze kwa mikono yao.

Akamaliza kwa kuwatakia busara katika ndoa na cha mno, katika migogoro wawe wa kusaka suluhu katika mazingira ya amani ndani ya
kusemezana na wawe wa kuridhiana na kusameheana.

Akiomba, akawatakia mema ya ndoa kwa kuwa “ni mapenzi ya Mungu walio katika ndoa wakae kwa amani na wabarikiwe kwa kila neema.”

You can share this post!

KASHESHE: Naandamwa na mafisi tu!

Pomegranate hukuzwa kurembesha mazingira ingawa matunda...

adminleo