LISHE: Sukumawiki na nyama ya mbuzi

Na MARGARET MAINA

mwmaina@ke.nationmedia.com

Muda wa kuandaa: Dakika 15

Muda wa mapishi: Dakika 40

Walaji: 4

Vinavyohitajika

 • nyama kilo 1
 • sukumawiki
 • karoti 2
 • pilipili 1
 • kitunguu maji
 • nyanya 3
 • nyanya ya kopo vijiko 2
 • kitunguu saumu (chukua vipande 5)
 • curry powder vijiko 2
 • chumvi
 • mafuta ya kupikia

Maelekezo

Katakata nyama na uioshe kabla ya kuiweka katika sufuria safi iliyobandikwa mekoni. Weka chumvi na tangawizi mbichi na upike hadi iive na kulainika.

Weka mafuta ya kupikia katika sufuria mekoni na yakishapata moto, katakata kitunguu maji halafu ukoroge kwa kupindua hadi kiive.

Osha pilipili uikatiekatie ndani halafu koroga vizuri. Ongezea curry powder na nyanya ya kopo na uendelee kukoroga vizuri. Weka chumvi.

Zile karoti zikwangue na utumbukize vipande ndani ya mboga yako kisha koroga.

Acha nyanya ziive.

Osha na ukate sukumawiki. Weka ndani halafu koroga vizuri kabla ya kuongezea nyama pamoja na dhania.

Koroga vizuri halafu uache kwa muda wa hadi dakika tano hivi.

Epua na pakua tayari kuliwa na sima.