• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Roma, Villarreal na Ajax waweka hai matumaini ya kufuzu kwa robo-fainali za Europa League msimu huu

Roma, Villarreal na Ajax waweka hai matumaini ya kufuzu kwa robo-fainali za Europa League msimu huu

Na MASHIRIKA

TIMU za Ajax, AS Roma na Villarreal ni miongoni mwa vikosi vilivyojiweka pazuri zaidi kufuzu kwa robo-fainali za Europa League msimu huu wa 2020-21 baada ya kubwaga wapinzani wao kwenye mechi za mkondo wa kwanza mnamo Alhamisi usiku.

Roma ambao ni miamba wa zamani wa soka ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) waliwakung’uta Shakhtar Donetsk ya Ukraine 3-0 katika uwanja wao wa nyumbani huku Ajax ya Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) pia wakiwapokeza Young Boys kutoka Uswisi kichapo cha 3-0 jijini Amsterdam, Uholanzi.

Villarreal ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) kwa alama 37, waliwakomoa Dynamo Kyiv ya Ukraine 2-0 huku Granada wanaokamata nafasi ya 10 kwenye jedwali la La Liga wakisajili matokeo sawa na hayo dhidi ya Molde ya Norway nchini Uhispania.

MATOKEO YA EUROPA LEAGUE (Machi 11, 2021):

Man-United 1-1 AC Milan

Slavia Prague 1-1 Rangers

Olympiakos 1-3 Arsenal

Tottenham 2-0 Dinamo Zagreb

Ajax 3-0 Young Boys

Dynamo Kyiv 0-2 Villarreal

Granada 2-0 Molde

Roma 3-0 Shakhtar Donetsk

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kiongozi mwenye nia njema afaa kurithi mikoba ya Rais...

PSG wafuatilia hali ya Ronaldo kambini mwa Juventus kwa nia...