• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 3:25 PM
Kampuni yaomba serikali kupunguza gharama ya umeme

Kampuni yaomba serikali kupunguza gharama ya umeme

Na SAMMY KIMATU

[email protected]

KIWANDA cha Halar Industries Limited ni moja ya kampuni kubwa ya usafishaji taka ya plastiki katika Kanda ya Afrika Mashariki.

Kampuni inafanya usafishaji wa aina nyingi za plastiki ambazo zinaweza kuchakatwa ikiwa ni pamoja na chupa za PET, Polythene, Plastiki Hard nk.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw Sagar Chandrakant Shah alisema janga la Covid-19 limeathiri vibaya biashara.

Kwa sababu ya nyakati ngumu za kiuchumi baada ya Covid-19, kampuni hiyo haikufuta wafanyakazi ila kuwaweza kazini zaidi ya wafanyikazi 300 wanaofanya kazi kwa zamu.

Bw Shah ameiomba serikali kupunguza gharama ya umeme na kudhibiti uingizaji wa bidhaa zilizomalizika kwani ni za bei rahisi kutokana na gharama yao ya uzalishaji ambayo ni ya bei ya chini.

Aidha, kutokana na uigizaji wa bidhaa za plastiki kutoka nchi zingine, kampuni ambazo hutengeneza bidhaa sambamba hapa Kenya hupata hasara kubwa kufuatia ushindani huo.

“Kati ya asilimia 30-40 ya matumizi ya kampuni hutumiwa na bili za umeme. Tunaomba msaada kutoka kwa serikali kupunguza gharama za umeme ambazo zinawezesha kuendeleza tasnia ya humu nchini Kenya,’’ Bw Shah alisema.

Aliongeza kuwa kampuni zinazotengeneza bidhaa kutoka plastiki kuukuu zinapaswa kupata motisha ya ziada kutoka kwa serikali ambayo alisema, inahitajika kuhamasisha watengenezaji wa bidhaa kutoka plastiki hapa Kenya.

Zaidio ya hayo, alisisitiza kuwa serikali inafanya kazi kubwa katika kukuza miundombinu kwa kujenga barabara, usafirishaji wa reli ambayo husaidia biashara masoko yanakopekekwa bidhaa.

Bw Shah alikuwa akizungumza jana kwenye chumba cha maonyesho cha kampuni hiyo katika eneo la Viwanda la Nairobi.

“Mbali na kuwa na wafanyikazi zaidi ya 300 katika kiwanda chetu, tumetengeneza ajira kwa watu zaidi ya 1,000 moja kwa moja na wengine kupitia mchakato huo kuanzia kwa ukusanyaji wa plastiki zilizotumika hadi hatua yake ya mwisho katika mauzo, ” Bw Shah aliambia Taifa Leo.

Lengo la kampuni, Bw Shah anasema, ni kusaidia kupunguza takataka mitaani na kuifanya nchi iwe safi na kutengeneza ajira zaidi kwa wenyeji kwa kutoa faida za kiuchumi kwa wanaohusika na taka.

Kampuni hiyo ina bidhaa mbalimbali wenye soko kuanzia Viti, ndoo, rula, mishumaa, vikombe, kamba na aina zingine za bidhaa za plastiki.

Bw Shah anawahimiza Wakenya kununua bidhaa nyingi zinazozalishwa hapa nchini na hiyo inaweza kusaidia kukuza tasnia yetu ya hapa na kutengeneza fursa zaidi za ajira kwa Wakenya.

Vilevile, anawahimiza pia Wakenya wanunue bidhaa ambayo inaweza kutumiwa tena na ina thamani ya pesa kwa mnunuzi.

You can share this post!

ODM, ANC kwenye mvutano wa ni nani ateuliwe naibu gavana...

Obado atishia kubomoa ngome ya Raila