• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Madai polisi walipata mamilioni kwa majaji

Madai polisi walipata mamilioni kwa majaji

Na RICHARD MUNGUTI

POLISI walipata zaidi ya Sh6.1 milioni katika afisi za majaji wawili wa mahakama kuu wanaochunguzwa kwa ufisadi Ijumaa wiki iliyopita.

Katika ushahidi uliowasilishwa kortini Alhamisi, Inspekta Felix Karisa Banzi alisema makachero walipata Dola za Amerika 57,000 (sawa na Sh6.1 milioni) katika afisi za Majaji Aggrey Muchelule na Said Juma Chitembwe.

Inspekta Banzi ambaye ni mchunguzi kutoka kitengo cha Uchunguzi wa Jinai (DCI), alisema polisi walipata pesa hizo baada ya kupekua afisi hizo.

Aliwasilisha ushahidi huo kupitia afisi ya Mwanasheria Mkuu, Dola 50,000 zilizopatikana katika afisi ya Jaji Muchelule na Dola za Marekani 7,000 katika afisi ya Jaji Chitembwe.

Kulingana na ushahidi uliowasilishwa katika kesi iliyowasilishwa na chama cha mahakimu na majaji nchini (KMJA), polisi walimpata mwanamke katika afisi ya Jaji Muchelule akiwa na pesa hizo.

Ushahidi umesema mwanamke huyo ni broka aliyefikishwa katika afisi ya Jaji Muchelule na Jaji Chitembwe. Kesi itasikilizwa Oktoba 21, 2021.

You can share this post!

China yavunja rekodi ya dunia kwenye uogeleaji wa 4x200m...

Shahbal asema bado hajaingia rasmi ODM