• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 6:36 PM
China yavunja rekodi ya dunia kwenye uogeleaji wa 4x200m relay kwa upande wa wanawake

China yavunja rekodi ya dunia kwenye uogeleaji wa 4x200m relay kwa upande wa wanawake

Na MASHIRIKA

CHINA walihimili ushindani mkali kutoka kwa Amerika na kuzoa dhahabu ya Olimpiki kwenye fani ya uogeleaji ya 4x200m freestyle relay baada ya kuvunja rekodi ya dunia jijini Tokyo, Japan.

Wapiga mbizi wa China walikamilisha pambano hilo kwa dakika 7:40.33 na kuvunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Australia kwa muda wa dakika 1:17.

Amerika (7:40.73) waliridhika na nishani ya fedha huku Australia wakijizolea shaba (7:41.29).

China walivuna ushindi huo baada ya mwogeleaji Zhang Yufei pia kuvunia taifa lake hilo nishani ya dhahabu kwenye 200m butterfly kwa upande wa wanawake.

Yufei, 23, aliandikisha rekodi mpya ya Olimpiki ya dakika 2:03.86. Regan Smith wa Amerika alijizolea medali ya fedha huku mwenzake Hali Flickinger akiridhika na nishani ya shaba.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kigogo Novak Djokovic ampepeta Nishikori na kutinga...

Madai polisi walipata mamilioni kwa majaji