• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:03 AM

Kindiki aamuru daktari gaidi atumikie kifungo cha miaka 12 kwa kupanga kuangamiza Wakenya

NA RICHARD MUNGUTI WAZIRI wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki amekataa jaribio la kupunguza kifungo cha miaka 12 dhidi ya gaidi aliyepanga kuangamiza Wakenya akitumia sumu ya kemikali ya virusi vya ugonjwa wa kimeta (Anthrax). Prof Kindiki aliamuru Dkt Mohamed Abdi Ali aliyefungwa na hakimu mkuu Martha Mutuku atumike kifungo chote. Waziri huyo alikataa kutumia […]

Maguire alivyokataa kugwaya na kuibuka mnara imara wa Man United msimu huu

 NA LABAAN SHABAAN HARRY Maguire alikejeliwa na mashabiki wa upinzani na timu yake kwandama. Akaishia kupokonywa unahodha. Ila, Maguire hakugwaya. Alisimama kidete akaweka kichwa juu na sasa yeye ni mnara katika ulinzi wa Manchester United. Difenda huyu alicheka na nyavu mara mbili katika mechi mbili zilizopita. Liverpool ilipochuana na United, alicheza kwenye safu ya mbele na […]

Serikali ilifanya vizuri kutuondolea jukumu la nidhamu kwa wanafunzi -Mwalimu

NA FRIDAH OKACHI WALIMU wengi nchini wanaepuka ugomvi na dharau kutoka kwa wazazi huku wakitumia mtindo wa kufunza na kisha kwenda nyumbani baada ya serikali kuondoa adhabu ya kiboko shuleni. Sheria ya Elimu kwenye Katiba Ibara ya 36, inasema kuwa hakuna mwanafunzi atakayefanyiwa ukatili, unyama au adhabu ya kudhalilisha kwa namna yoyote ile, iwe ya kimwili […]

Unavyoweza kutahadhari usipatwe na janga mafuriko yanapotokea

NA LABAAN SHABAAN HUKU mvua kubwa ikiendelea kuponda sehemu nyingi nchini, Shirika la kutoa misaada la Red Cross limeorodhesha ushauri kwa Wakenya kuepuka madhara. Maeneo yanayoathiriwa na mafuriko ni ukanda wa Ziwa Victoria, Bonde la Ufa, Kusini Mashariki, Pwani, Kaskazini Mashariki na Nairobi. Sambamba na serikali, Red Cross inashauri Wakenya wanaoishi nyanda za chini kuhamia […]

Ndani ya ziara ya Ruto nchini Tanzania, akutana na mvua huko

NA MARY WANGARI RAIS William Ruto mnamo Ijumaa aliungana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu kusherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa iliyokuwa Tanganyika na visiwa vya Zanzibar huku ziara yake nchini humo ikiibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya. Rais Ruto aliondoka Alhamisi usiku kujumuika na Watanzania katika sherehe hizo kabla ya kusafiri nchini […]

Watu saba waokolewa baada ya lori lao kusombwa na mafuriko

NA MWANDISHI WETU WATU saba wameokolewa kutoka kwa Mto Kwa Muswii na kupelekwa katika hospitali ya Sultan Hamud, Shirika la Msalaba Mwekundu nchini, Kenya Red Cross, limesema Ijumaa. Limeongeza kwamba shughuli ya uokoaji inaendelea. Inakadiriwa watu 10 walitumbukia majini baada ya lori kusombwa na mafuriko wakijaribu kuvuka Mto Muswii katika Kaunti ya Makueni. Katika mojawapo […]

Liverpool kwenye mizani ya West Ham United

NA MASHIRIKA LONDON, UINGEREZA LIVERPOOL watasonga hadi nafasi ya pili kwenye jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) kwa saa kadha iwapo wataruka kamba ya wenyeji West Ham United katika uwanja wa London Stadium, Jumamosi alasiri. Nao Manchester United watakuwa nyumbani dhidi ya Burnley baadaye Jumamosi jioni kutafuta ushindi utakaoimarisha matumaini yao ya kumaliza sita-bora […]

Magavana wakaa ngumu, wanataka mgao wa Sh439bn kuwasitiri dhidi ya ushuru wa juu

Na COLLINS OMULO MAGAVANA wamekataa mgao wa bajeti wa Sh391.1 bilioni uliopitishwa na wabunge wakishikilia kuwa hawatakubali mgao usiopungua Sh439.5 bilioni. Wakuu hao wa serikali za kaunti wanasema kuwa wanakabiliwa na gharama nyingine za lazima ambazo zitaongeza kwa Sh20 bilioni kiasi cha pesa wanazohitaji kugharimia mahitaji ya serikali zao katika mwaka unaokamilika Juni 2025. Mwenyekiti […]

Takriban watu 10 wasombwa na maji wakijaribu kuvuka mto wakiwa ndani ya gari Makueni

NA PIUS MAUNDU TAKRIBAN watu 10 wanashukiwa kuangamia baada ya kusombwa na mafuriko walipokuwa wanajaribu kuvuka Mto Muswii katika Kaunti ya Makueni. Katika mojawapo ya video ambayo imenaswa na walioshuhudia, abiria waliokuwa kwenye gari lililozama wanaonekana wakijaribu kuogelea huku maji yaliyokuwa yanaenda kwa kasi yakiwalemea huku waliokuwa wanatazama wakipiga mayowe. Hakukuonekana waliojaribu kuwaokoa kwa hofu […]

Watu 155 waaga dunia TZ kufuatia mafuriko, maporomoko ya ardhi

NA MASHIRIKA DAR ES SALAM, TANZANIA WATU 155 wamepoteza maisha na wengine 236 kujeruhiwa kufuatia mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Tanzania, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Kassim Majaliwa amesema. Majaliwa aliliambia Bunge la Tanzania kwamba mafuriko hayo yanayosababishwa na mvua ya El Nino inayoshuhudiwa katika ukanda wa Afrika Mashariki pia […]

Atwoli aruhusu Fazul akague matumizi ya fedha za ‘masoja’

Na CHARLES WASONGA LENGO la kwanza la Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Nchini (COTU), kulingana na maelezo kwenye tovuti yake, ni kuinua hali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ya wafanyakazi wote nchini. Aidha, muungano huo unasema shughuli zake zote huwa zinalenga kuangazia matakwa ya wafanyakazi katika ngazi ya kitaifa, kanda na kimataifa. Isitoshe, COTU hulenga […]