• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM

Shule kufunguliwa Jumatatu kuanza muhula wa pili

NA CHARLES WASONGA RAIS William Ruto ametangaza Jumatano kuwa shule zote nchini zitafunguliwa rasmi Jumatatu, Mei 13, 2024, kuanza kwa masomo ya muhula wa pili. Akiongea alipokutana na ujumbe wa viongozi kutoka maeneobunge ya Laikipia Kaskazini na Kajiado ya Kati, Dkt Ruto alisema kuwa hatua hiyo inatokana na ushauri kutoka kwa Idara ya Utabiri wa […]

Abiria wamechoka: Bodaboda wasiooga wamulikwa

NA MWANGI MUIRURI WAHUDUMU wa bodaboda eneo la Mlima Kenya wamezindua msako wakilenga wenzao ambao wamegomea maji msimu huu wa kijibaridi kikali kinachotokana na mvua ya maangamizi. Hii ni baada ya malalamishi kutolewa kwamba baadhi ya wahudumu wa bodaboda hunuka kama panya aliyeoza. Abiria ambao ni kawaida katika uchukuzi wa aina hiyo kukaa karibu na […]

Miradi Lamu yaachia wenyeji kicheko na kilio kwa wakati mmoja

NA KALUME KAZUNGU INAAMINIKA kwamba mara nyingi miradi ya maendeleo inapofika au kuanzishwa mahali, basi eneo hilo huishia kukua na kupanuka. Yaani kubuniwa kwa miradi mahali ni sawa na msemo wa ‘Mgeni Njoo Mwenyeji Apone’. Na ndio sababu pindi mradi unapotua mahali, utapata miundomsingi muhimu kama vile barabara ambayo awali haikuwapo, ikianza kujengwa. Pia utapata […]

Sauti ya mnyonge kila kona

NA WAANDISHI WETU IDADI ya Wakenya wanaohitaji usaidizi wa dharura kwa mahitaji ya kimsingi iliendelea kuongezeka jana baada ya serikali kuanza kubomoa makazi yanayokaribiana zaidi na mito. Serikali ilichukua hatua hiyo kama sehemu ya mkakati mpana wa kuepusha maafa na hasara inayosababishwa na mafuriko. Kila nyumba iliyo ndani ya mita 30 kutoka ukingo wa mto […]

Mafuriko: Mgawanyiko wa kitabaka shule za kibinafsi zikiendelea na masomo kidijitali

NA DAVID MUCHUNGUH HATUA ya kuahirisha ufunguzi wa shule hadi tarehe isiyojulikana imeibua mgawanyiko wa kitabaka huku watoto kutoka familia maskini, wengi wao wanaosomea shule za umma, wakiendelea bila masomo wenzao kutoka familia tajiri wakisoma kidijitali. Shule za umma zimeathirika zaidi licha ya serikali kutumia zaidi ya Sh32 bilioni kuzinunulia tableti, vipakatalishi, projekta, vifaa vya […]

Eliud Kipchoge: Simwamini mtu yeyote… hata kivuli changu

NA LABAAN SHABAAN BINGWA mara mbili wa mbio za masafa marefu katika mashindano ya Olimpiki Eliud Kipchoge anasema hana imani na mtu yeyote, hata kivuli chake. Mwanariadha huyo katika mahojiano na BBC Sport Africa, alifichua aliingiwa na kiwewe huku akihofia usalama wake na wa familia yake, baada ya kuhusishwa na kifo cha mshikilizi wa rekodi […]

Mungiki wadaiwa kutesa, kuibia abiria Karatina

NA MWANGI MUIRURI WAHUNI wanaofungamanishwa na kundi haramu la Mungiki sasa wanadaiwa kuteka nyara mji wa Karatina ambao ni ngome kuu ya Naibu Rais, Rigathi Gachagua. Imeripotiwa kwamba wahuni hao hushika doria katika maeneo kadha ya mji huo hasa katika steji za uchukuzi na pia kwa madanguro. Kwenye ripoti moja ambayo Taifa Leo imeona katika […]

Borussia Dortmund yasubiri Bayern au Real Madrid

Na MWANGI MUIRURI KLABU ya Borussia Dortmund mnamo Jumanne iliibandua nje Paris Saint Germain (PSG) katika hatua ya nusu-faijali ya Klabu Bingwa Ulaya (Uefa) kwa kuikung’uta bao 1-0. Bao la Mats Hummels katika dakika ya 50 ndilo lilizika PSG katika kaburi la sahau la Uefa kwa msimu huu, ikitumwa kujaribu bahati katika msimu ujao. Timu […]

Mkewe Mwangi Wa Iria ajipata pabaya kwa ufisadi wa Sh351m

NA RICHARD MUNGUTI MKEWE aliyekuwa Gavana wa Murang’a Mwangi wa Iria, Jane Waigwe Kimani ameshtakiwa kwa kula njama za kuilaghai kaunti hiyo zaidi ya Sh351 milioni. Jane alishtakiwa mbele ya hakimu mkuu Victor Wakhumile katika mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Milimani. Mkewe huyo gavana wa kwanza kaunti ya Murang’a, alishtakiwa pamoja na Bw David […]