• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
DONDOO: Bodaboda ashtua demu kufika kwake alfajiri na kumtaka amfungulie

DONDOO: Bodaboda ashtua demu kufika kwake alfajiri na kumtaka amfungulie

NA NICHOLAS CHERUIYOT

Mrembo wa hapa, aliudhika mwanabodaboda alipofika kwake saa kumi na moja ya asubuhi ilhali alikuwa amemtaka afike saa kumi na mbili unusu asubuhi.

Kulingana na duru, kipusa alikuwa na safari ya mbali na alimtaka jombi afike kwake asubuhi kumbeba hadi steji ya mabasi.

Kipusa huyo anayeishi pekee yake alishtuka kusikia sauti ya pikipiki mapema mno akiwa bado kitandani.

“Hodi! Hodi! Nimefika sasa. Nifungulie, huku nje ni baridi mno,” mwendeshaji pikipiki alibisha mlangoni.

“Mbona umekuja mapema mno? Una nia gani. Hata sijaamka,” kipusa akalalamika.

Tetesi za polo aruhusiwe ndani ya nyumba kumsubiri demu aoge hazikufaulu kwani kipusa alikataa katakata.

***

Kizaazaa pasta akiweka Biblia kando na kumlima jamaa aliyemtorosha mkewe

NA CORNELIUS MUTISYA

Kisanga kilishuhudiwa mjini hapa, pasta mmoja alipoweka Bibilia chini na kumtwanga jamaa aliyetorosha mkewe.

Jamaa huyo alikuwa akifanya kazi nyumbani kwa mhubiri huyo na akaanzisha uhusiano wa kimahaba na mkewe.

Inadaiwa mapenzi yao yalinoga mno na wakatoroka wakaenda kuishi pamoja katika chumba cha kupanga mjini hapa.

Juzi, pasta alikutana na jamaa huyo mjini hapa na wakaanza kupigana akimtaka amweleze alikokuwa mkewe.

Ilibidi wananchi waingilie kati na wakawatenganisha kabla ya kuchafuana sura zaidi.

“Pasta fahamu kuwa maji yakimwagika hayazoleki. Itakubidi uzoee,” mama mmoja alimtania pasta.

***

Demu aomba mumewe radhi kushiriki uganga kusaka mtoto wa kiume

NA DENNIS SINYO

MWANAMKE mmoja alimuomba mumewe msamaha kwa kutafuta huduma za mganga ili ajaliwe mtoto wa kiume bila kumjulisha.

Mama huyo alikuwa amepata watoto 5 wasichana huku juhudi zake za kupata mtoto mvulana zikiambulia patupu.Baada ya presha ya kupata mtoto mvulana kuzidi,mama huyo aliamua kutafuta msaada kwa mganga.

Hata hivyo,juhudi zake zilionekana kugonga mwamba baada ya kushindwa kupata mvulana.

Baada ya kugonga mwamba,mama huyo aliamua kumjulisha mumewe kuhusu safari zake kwa mganga na kuomba msamaha kwa kuweka siri hiyo kwa muda mrefu.

  • Tags

You can share this post!

Wauguzi 66 watuzwa kwa kazi nzuri ya kuwashughulikia...

Subirini kidogo tu, hali itakuwa shwari, Ruto ahakikishia...

T L