• Nairobi
  • Last Updated May 15th, 2024 8:55 PM
Subirini kidogo tu, hali itakuwa shwari, Ruto ahakikishia Wakenya kuhusu hali ngumu ya maisha

Subirini kidogo tu, hali itakuwa shwari, Ruto ahakikishia Wakenya kuhusu hali ngumu ya maisha

NA ERIC MATARA

RAIS William Ruto Ijumaa, Oktoba 20, 2023 alisisitiza kuwa mpango wa kuwekeza bajeti katika kilimo umeanza kuzaa matunda, na kwamba hivi karibuni bei ya vyakula itapungua.

Kiongozi wa nchi alisema wakati wa sherehe za Mashujaa mjini Kericho kwamba kupunguza bei ya mbolea kutoka Sh7,000 hadi Sh2,500 kunatarajiwa kusaidia wakulima kuvuna magunia 61 milioni ya mahindi mwaka huu.

Kulingana na Rais, hili litakuwa ongezeko la karibu asilimia  hamsini ya mavuno ikilinganishwa na mwaka jana, 2022.

“Ndio sababu juhudi zetu katika kupunguza gharama ya maisha zitafanikiwa. Tumejikita zaidi katika kuongeza uzalishaji wa kilimo na kupanua kiwango cha ardhi kinachotumika kuzalisha chakula,” akasema.

Mbolea ya bei nafuu ndio mpango pekee kwa kuwapa afueni wananchi, ambao serikali ya Kenya Kwanza iliudumisha kutoka kwa serikali iliyotangulia.

Usambazaji wa fatalaiza ya bei nafuu ulizinduliwa mapema 2023, kupitia mpango wa ruzuku ya mbolea.

 

  • Tags

You can share this post!

DONDOO: Bodaboda ashtua demu kufika kwake alfajiri na...

Jombi ashindwa kula siku tatu baada ya kugundua aliyepanga...

T L