• Nairobi
  • Last Updated May 29th, 2023 9:37 PM
Kisura azua fujo kwa kalameni akidai Sh5,000 zamshusha bei

Kisura azua fujo kwa kalameni akidai Sh5,000 zamshusha bei

UKUNDA,KILIFI

Na DOMINIC MAGARA

KIDOSHO mmoja alikataa kushuka kutoka gari la windo lake akidai kulipwa Sh 10,000 kama ada ya kukesha kwa jamaa. Wawili hao walishambuliana ndani ya gari nusra wasababishe ajali mbaya karibu na kituo cha magari cha Ukunda.

Soja wa ploti alidokeza kuwa, mrembo alifika kwa jamaa kwa teksi. Walikesha wakila uroda na asubuhi walipoingia kwa gari la jamaa, aliwasikia wakigombana wakirushiana maneno makali, kila mmoja akitaja hesabu yake. Baadaye gari liliondolewa kwa kasi na kusimama ghafla katikati ya barabara.

Wawili hao walishikilia ushukani kila mmoja akivuta upande wake. Dada alipiga kelele na kulaani malipo ya Sh 5,000. “Nilipita kulipwa Sh5,000 miaka mingi iliyopita, ongeza pesa hapa,’’ alisikika akiwika.

Juhudi za jamaa kujitetea hazikufaulu. Mrembo alichomoa funguo za gari na kuziweka kipochini.

You can share this post!

Mianya ya pembejeo bandia yazibwa kampuni zikikumbatia...

CECIL ODONGO: Mudavadi ataingia ikulu rahisi kupitia kwa...

T L