• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM

Na JOHN KIMWERE 
NI miongoni mwa wasanii chipukizi wa kike wanaozidi kuvumisha jukwaa la burudani kupitia uigizaji na vichekesho hapa nchini.
Aidha ni kati ya wanamaigizo wanaopania kujituma kiume kuhakikisha wametinga upeo wa kimataifa miaka ijayo. Evalyne Wanja Mwangi maarufu kama Eve ni  mjasiriamali na produsa ambaye kitaaluma alianza kujituma katika masuala ya uigizaji mwaka jana.
”Hata hivyo nilianza kushiriki uigizaji kama burudani miaka nane iliyopita,” binti huyu anasema na kuongeza kuwa filamu ya Nairobi Half life ilimtia motisha zaidi kuendeleza talanta yake katika uigizaji ambayo haikuwa imetambuliwa.
Pia anasema kazi zake kati ya waigizaji shupavu afrika, Davis Viola ilizidisha hamu yake kujiunga na sekta ya maigizo. Mwanzo wake baada ya kutamatisha elimu ya kidato cha nne mwaka 2013 alijiunga na kundi la ISCEBEE Funs.
Ingawa hajapata mashiko katika tasnia ya uigizaji anajivunia kushiriki zaidi ya filamu kumi ambazo mbili yazo zimepata mpenyo na kupeperushwa kupitia Maisha Magic TV. ”Hakika nilijiunga na uigizaji mwaka uliyopita lakini nimepiga hatua kiasi ambapo nimeshiriki filamu kama  ‘Varshita’ na ‘Selina’ zilizopeperushwa kwenye runinga.
Zingine bado hazijapata mpenyo ikiwamo Death Night ambayo ndio aliyoshiriki kwanza kabisa. Aidha zipo ‘Ella,’ ‘White feather,’ ‘Mucii,’ ‘Contrition,’ ‘Tapeli,’ ‘Salama Monoloques,’ ‘Death Night,’ na ‘A strangers House,’ kati ya zingine. Kama produsa amezalisha filamu iitwayo ‘Wingu’ anaposema analenga kumiliki brandi yake hivi karibuni.
Picha/JOHN KIMWERE
Evalyne Wanja Mwangi maarufu kama Eve
  Jo-Issa Rae Diop
Ninaamini uigizaji ni ajira ninayolenga kutumia kama kitenga uchumi maishani mwangu huku nikipania kufuata nyayo zake kati ya waigizaji mahiri duniani Jo-Issa Rae Diop mzawa wa Marekani. Msanii huyo aliye pia mwandishi na produsa ameshiriki filamu kama ‘Little,’ ‘Insecure,’ ‘Love Birds,’ na ‘The Hate you give,’ kati ya zingine.
Chipukizi huyu anasema anajiona akishiriki filamu za Wollywood ndani ya miaka mitano ijayo. ”Aidha ndani ya muda huo natumai nitakuwa namiliki brandi yangu na kuzalisha angalau filamu mbili,” akasema.
Dada huyu anatoa mwito kwa serikali ikome kuzitoza ushuru wa juu kampuni za kigeni zinapohitaji kufanyia kazi ya uigizaji humu nchini. ”Sio siri tena inafahamika kuwa endapo serikali inaweza kuweka sera za kufaidi wahusika katika tasnia ya ugizaji nchini inaweza kutoa ajira kwa wasanii wengi tu wanaume na wanawake,” akasema.
 
Mawaidha
Anashauri wanadada wenzie wasijiunge na sekta hii kusaka umaarufu bali wafahamu wanachotafuta maishani. Pia anawaambia lazima wajitolee kuhudhuria majaribio (auditions) maana hakuna kazi itakayowakuta kwa nyumba pia wasipuuze brandi ndogo ndogo kwa kuzingatia hakuna anayefahamu bahati yake itatua lini.
”Ni muhimu kwetu kuwa wavumilivu, kujituma pia tuwe wabunifu ili kuibuka bora katika tasnia ya uigizaji,” alisema.
Picha/JOHN KIMWERE
  • Tags

You can share this post!

Christina Munyao anavyovumisha tasnia ya filamu nchini

Argentina waangusha Paraguay huku Chile wakitoka nguvu sawa...