• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 7:55 PM
Christina Munyao anavyovumisha tasnia ya filamu nchini

Christina Munyao anavyovumisha tasnia ya filamu nchini

Na JOHN KIMWERE

NI kati ya wasanii wa kike walioamua kuvumisha tasnia ya filamu nchini.

Alianza kujituma kwenye masuala ya filamu mwaka 2014 baada ya kukamilisha elimu ya kidato cha nne. Dah! Unajua nini? Wahenga kweli hawakupaka mafuta kwenye mgongo wa chupa walivyolonga kuwa ‘Vitu vya biashara havigombani.

Christina Munyao ambaye kisanaa anafahamika kama Tina Clara amepania kuibuka kati ya waigizaji wachanga wanaomiliki brandi za kuzalisha filamu nchini. Binti huyu ni mwigizaji wa kujitegemea anayejivunia kushiriki zaidi ya filamu ambazo baadhi yazo zimepeperushwa kupitia vituo tofauti ikiwamo Citizen TV na KBC kati ya zingine.

”Hakika mipango ya Mungu hakuna anayeweza kuibadilisha. Nilijiunga na uigizaji kimuujiza maana produsa aligundua kipaji changu baada ya kumpeleka rafiki yangu kushiriki majaribio (audition),” anasema na kuongeza kuwa aliteuliwa na kumshinda mwenzake huyo aliyemshukiwa mpaka leo.

Tyler Perry

Chipukizi huyu amehitimu kwa shahada ya digrii katika masuala ya uigizaji na amevalia kofia nyingi tu katika sekta ya sanaa ya burudani. Ingawa alianza kwakushiriki filamu za mwongozo wa vitabu vya riwaya (setbooks) leo hii ameiva kinoma.

Kipusa huyu aliyezaliwa mwaka 1997 ni mwana maigizo, video vixen, produsa na mwandishi wa script. Hayo tisa. Kumi analimiki brandi yake iitwayo Tina Tales anayopania kuifikisha upeo wa juu kama Tyler Perry Studios yake Tyler Perry mzawa wa Marekani.

 Picha/JOHN KIMWERE
Christina Munyao ambaye kisanaa anafahamika kama Tina Clara

”Ingawa tangia nikiwa mtoto nilidhamiria kuwa muimbaji ama mtangazaji wa runinga enzi hizo nilivutiwa na filamu za miongoni mwa waigizaji mahiri nchini India, Priyanka Chopra,” alisema na kuongeza kuwa sanaa ya maigizo ameibuka ajira anakolenga kufanya mambo miaka ijayo.

Metipso TV

Anajivunia kushiriki filamu nyingi tu ikiwamo kipindi cha Inspekta mwala ambacho hupeperushwa kupitia runinga ya Citizen TV pia kamba school series iitwayo Tr Makombo kwenye Viusasa. Aidha ameshiriki kipindi cha KCB GO Ahead TVC pia filamu kwa jina Pain and Love iliyopeperushwa kupitia kituo cha K24.

Kadhalika huandaa kipindi cha runinga ya mtandaoni ya Metipso TV kiitwacho Tina and The City. ”Kwa sasa ninatengeneza filamu mbili ambazo nimeziandika mwenyewe ‘Bella na Exile’ ambazo ninatarajia zitakuwa tayari baadaye mwaka huu,” akasema.

Kwa waigizaji wa kimataifa anatamani kujikuta jukwaa moja nao Thuso Mbedu(Afrika Kusini) na Mghana, Nadia Buari walioshiriki ‘Isibaya,’ na ‘Darkness of Sorrow,’ mtawalia kati ya zingine.

Mawaidha

Msichana huyu anashauri wenzie kuwa wasijiunge na uigizaji endapo hawana roho za kuvumilia maana shughuli sio mteremko jinsi wengine hudhania. ”Nawaonya kina dada wenzangu kuwa kamwe wasiwe na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wanapiga shughuli katika tasnia ya uigizaji pia wasizae kabla ya ndoa maana maisha yanazidi kuwa magumu,”’ akasema.

Anataka wenzie wanaokuja wawe wabunifu endapo wanapania kupenya katika sekta ya maigizo. Anadokeza kuwa kama sivyo ni rahisi kwa kuangukia meno ya maprodusa ambao hupenda kuwashusha hadhi wasanii wa kike.

 Picha/JOHN KIMWERE

  • Tags

You can share this post!

Kemri FC yaapa kupambana mwanzo mwisho