• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 7:02 PM
AAR kutoa huduma za afya katika eneo pana la Tatu City

AAR kutoa huduma za afya katika eneo pana la Tatu City

NA LAWRENCE ONGARO

AAR Healthcare wamejitolea kushirikiana na Tatu City kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa walengwa.

Shirika hilo litakuwa na ambulansi ya kisasa ambayo itakuwa na vifaa vyote vya matibabu.

Kulingana na mkataba huo, shirika hilo litahudumia wakazi wa Tatu City, wafanyabiashara, na wageni wanaozuru eneo hilo.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa Tatu City Bw Preston Mendenhall, ushirikiano huo ni muhimu kwa sababu kila mwananchi anayeishi eneo hilo atapata nafasi ya huduma za afya za dharura kupitia AAR Healthcare.

“Tuna imani ya kwamba afya ya kila mmoja itatiliwa maanani kwa sababu huduma ya matibabu itakuwa wazi,” alisema Bw Mendenhall.

Afisa mkuu wa usimamizi wa maswala ya Tatu City Perminas Marisi alisema Tatu City inazingatia afya ya kila mmoja na kwa hivyo wana imani kuwa shirika hilo la afya litatoa huduma za kupigiwa mfano.

Meneja mkuu wa AAR Healthcare Bi Elizabeth Wasunna, madaktari na wahudumu wao wengine wana vifaa vya kisasa vinavyoweza kusaidia kuokoa maisha ya wengi hata wakati wa dharura.

“Tuko tayari kutoa huduma kwa kila mmoja ambaye anahitaji. Madaktari na wahudumu wa AAR ni wale wenye ujuzi wa hali ya juu,” alisema meneja huyo.

Kwa wakati huu Tatu city inahifadhi wakazi wapatao 9,000 maeneo ya kibiashara yakiwa 75.

Baadhi ya kampuni zinazoendesha shughuli zao katika eneo hilo ni Copia, Cooper K- Brand, Twiga Foods,  Freight Forwarders Solution, na Kenya Wine Agencies Ltd (KWAL).

Kuna shule za msingi na upili ambazo idadi jumla ya wanafunzi ni  3,500.

  • Tags

You can share this post!

Wazee wa vijiji kutambuliwa rasmi kisheria

Utalii Lamu wayumbishwa na Al-Shabaab

T L