• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 5:23 PM
Ana maono ya kucheza soka ya kulipwa

Ana maono ya kucheza soka ya kulipwa

NA PATRICK KILAVUKA

KUJIAMINI, nidhamu,ujasiri na kuonyesha weledi kulimpa safu ya ukipa na hifadhi Alexander Mikisi, 21 katika ngome ya timu ya Potters FC ya Githogoro, kaunti ndogo ya Westlands.

Anasema aliamini palipo na nia kuna njia alipotua jijini Nairobi.Mdakaji Mikisi ambaye alikuwa mchezaji tangu akiwa Shule ya Msingi ya St. Louis Saisi, Makutano, kaunti ndogo ya Lugari. Isitoshe, aliendelea kujikuza zaidi akiwa Sekondari ya Savala.

Aliifikisha timu ya shule yake ya upili kiwango cha Kaunti ya Kakamega akiwa kidato cha nne mnamo 2018.Kwa vile ujuzi huongezewa maarifa, alishiriki pia katika kambini ya timu ya Makutano Soccer Academy, Lugari ambayo ilikuwa mlezi mbadala chini ya kocha Stephen Imbinda akiwa katika kikosi cha wasiozidi miaka 14.

“Mkufunzi Imbinda aliniongezea ncha ya maarifa kwani aliniweka katika mkondo mkali wa maozezi na nidhamu. Hali hiyo, ilinimakinikisha sana katika safu ninayoishikilia na ninafurahia kwani maelekezo yake yalikuwa taa ya kipaji changu,” asema mnyakaji huyo ambaye kwa sasa ameaminiwa nafasi hiyo na mkufunzi wa Potters Erick Amalele ambaye alimsajili 2019 baada tu ya kuhudhuria zoezi la kujinoa na jicho pevu lake likamtambua.

Kocha Erick alisema kwamba kipa Mikisi ni mdakaji wa ajabu kwa sababu tangu aiingie timuni wakiwa Ligi ya Kauntindogo ya Shirikisho la Soka Kenya baada ya kutia wino, amebadilisha timu kwa kuwa komeo tosha hadi timu imepandishwa ngazi kushiriki Ligi ya Kaunti msimu huu “Sikuweza kuamini nilipomjaribu! Alionyesha ni mweledi katika kuchapa shughuli ya ukipa.

Ni mwanasoka anayejiamini, mwenye nidhamu na mjasiri. Hupanga timu kuziba nyufa kwenye safu ya ulinzi barabara, ” akasema kocha huyo wakati wa mahojiano na kuongezea kwamba, huwa radhi kufia timu na ana pasi za uhakika anapopiga mpira.

Mkamataji boli Alexander alirithi kipaji cha kabumbu kutoka kwa babaye Jafredy Musee Mikisi ila, angependa kucheza mithili ya kipa Patrick Matasi ambaye aliwahi kushikia AFC Leopards na kipa Thibaut Courtois wa Real Madrid ughaibuini.

Ungali muuliza timu gani angependa kuisukumia gurudumu la kandanda?  Yu radhi kusema kwamba angependa kuwa mchumani wa timu ya AFC Leopards na Manchester United  kwa sababu ya ushirikiano uliomo katika timu hizo na ari yao ya kupigania ushindi.

Changamoto amewahi kupata ni wakati walikuwa wanacheza dhidi FC Talents ambapo mchakato ulikuwa wa kasi na alifanyishwa kibarua lango kuwadhibiti wapinzani.
Anasema angependa kucheza soka ya kulipwa ughaibuni na kuvikuza vipawa mashinani kama njia kustawisha talanta zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Mamilioni ya fedha Kenya imetumia katika Safari Rally...

Waiguru aitaka Hazina ya Kitaifa kutoa fedha za Mei na Juni...