• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Ashtakiwa kwa kumchoma ‘ex’ kwa maji moto

Ashtakiwa kwa kumchoma ‘ex’ kwa maji moto

NA RICHARD MUNGUTI

MWANAUME ameshtakiwa kumchoma kwa maji moto mkewe waliyetengana.

Ezekiel Kikwatha alifunguliwa shtaka la kumuumiza Betty Mwathi mnamo Septemba 3, 2022 katika mtaa wa Pangani.

Kikwatha alikana shtaka la kumuumiza Betty kinyume cha sheria nambari 251 ya sheria za uhalifu.

Wawili hao inadaiwa walikuwa wametengana na kila mmoja alikuwa anaishi kwa nyumba yake.

Betty alirejea kutoka kanisani siku hiyo na kumpata Kikwatha akitazama mtandao kwa simu yake.

Betty alimuuliza Kikwatha alichokuwa anafanya kwa nyumba yake ilhali walikuwa wametengana.

Mshtakiwa alimrukia Betty akimrushia masumbwi na makofi na mateke.

Jaribio la Betty kutwaa simu yake halikufua dafu.

Mshtakiwa alichukua birika iliyokuwa na maji moto na kummwagia Betty.

Alichomeka kisha akatoroka na kuenda hospitalini.

Hatimaye Kikwatha alikamatwa.

Mshtakiwa alimsihi hakimu mkuu mahakama ya makadara Francis Kyambia amwachilie kwa dhamana ili asuluhishe kesi hiyo nje ya mahakama.

Mshtakiwa aliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000.

Akishindwa kupata dhamana hiyo mshtakiwa alipewa dhamana ya pesa taslimu Sh20,000.

Bw Kyambia aliorodhesha kesi hiyo itajwe Juni 13 na kutenga Julai 5 siku ya kuisikiliza.

  • Tags

You can share this post!

DOUGLAS MUTUA: Mwafrika awe suluhisho la ubaguzi wa rangi...

Kenya yashinda riadha za Afrika Mashariki nchini Tanzania

T L